KIKOSI
cha zima moto na uokoaji katika Manispaa ya Iringa kimeamua
kufikisha malalamiko yake kwa jeshi la polisi kufuatia mchezo mchafu
unaofanywa na baadhi ya watu kupiga simu za utoaji wa taarifa za
uongozi za kuwepo kwa moto hewa.
Akizungumza leo mtandao huu wa matukiodaima.co.tz mara baada ya kufika eneo la Zizi
la Ng'ombe nje kidogo ya mji wa Iringa kaimu mkuu wa kikosi cha
Zima moto na uokoaji mjini Iringa Juma Joseph alisema kuwa
walipigiwa simu majira ya saa 5 asubuhi kuombwa kufika eneo hilo
kuwa kuna nyumba inawaka moto ila baada ya kufika hawakuweza kuta
moto huo wala mtu aliyewapigia simu.
"
Kumekuwepo na mchezo wa baadhi ya wananchi wa mji wa Iringa
kupiga simu ofisi za Zimamoto kwa lengo la kutuchezea akili zetu
na baadhi wamekuwa wakipiga simu ili mradi kusikia sauti zetu na
kukata simu huku wengine wakitoa taarifa hewa za moto"
Alisema
matukio kama hayo yameendelea kuongezeka na kwa hilo tukio la Zizi
la Ng'ombe baada ya kufika eneo hilo namba iliyotumika haikuweza
kupatikana na wenyeji wa eneo hilo kudai hakuna tukio la moto katika
nyumba hiyo waliyoelekezwa,
Hivyo
alisema kutokana na tukio hilo wameona ni vema kwenda polisi ili
kuikabidhi namba hiyo kwa ajili ya kumsaka mhusika huyo na
kuchukulia hatua pamoja na kurudisha gharama za mafuta ambayo gari
hilo limetumia .
Alisema
mbali ya kutumia mafuta ya gari hilo pia jumla ya pikipiki mbili
za askari wa zimamoto zilitumika kwenda eneo la tukio haraka
zaidi ili kufanya shughuli ya uokoaji ila hakukuwa na moto wowote.
Kiongozi
huyo aliwaonya wananchi wa mji wa Iringa kuepuka kupiga simu za
kuwatania Zima moto kwani wakati mwingine mwenye mchezo huo anaweza
kuwa na tatizo kweli na moto na zimamoto wakajua ni utani wa siku
zote |
No comments:
Post a Comment