KAMANDA WA JESHI LA POLISI AKITOKA KWENYE UKUMBI WA POLISI NJOMBE
SACP FULGENCE NGONYANI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA WAMILIKI WA MALI WALIOFIKA KUTAMBUA MALI KATIKA OFISI ZA JESHI HILO
SACP FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE
JOSHUWA MWALONGO AKIWA NA MWENZAKE SALMU HONGORI ALIYEVAA SWETA LA POLISI WAKIWA WAMETIWA MBALONI KWA MAKOSA HAYO
HIZI NI MALI WALIZOKUTWA NAZO WATUHUMIWA MBALIMBALI WALIOKAMATWA KWENYE MSAKO WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE WA KUWASAKA WAHARIFU
WANANCHI WALIOKUTWA NA MATATIZO YA KUIBIWA MALI ZAO WAMEFIKA KATIKA OFISI ZA POLISI MKOA WA NJOMBE KUBAINI MALIZI ZILIZOPO
HIVI NI VITU VILIVYOIBIWA MAENEO MBALIMBALI NA SASA VIKIWA KITUONI HAPO NA WANANCHI BADO WANARUHUSIWA KUENDELEA KWENDA KUTAMBUA MALI ZAO
HAWA NI WANANCHI WALIOFIKA KUTAMBUA MALI HIZO
Na Michael Ngilangwa-Njombe
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia Watu 12 Wanaosadikika Kuwa Ni
Majambazi Sugu Wa Kutumia Silaha Ambao Wamekamatwa Katika Oparesheni
Iliyofanyika Kwa Kipindi Cha Siku Mbili Mnamo Octoba 1 Na 2 Mwaka Huu Katika
Maeneo Mbalimbali Ya Mkoa Wa Njombe.
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Pamoja Na Wamiliki Wa Mali Mbalimbali
Zilizokamatwa Kwenye Msako Huo Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe SACP
Fulgence Ngonyani Amesema Kuwa Watuhumiwa Hao 12 Sugu Wamekamatwa Kwa
Makosa Mbalimbali Ikiwemo Uvunjaji,Kupatikana Na Silaha,Kucheza Kamali,Wizi Wa
Mifugo Na Kukutwa Na Mali Mbalimbali Ambazo Zinadhaniwa Ni Za Wizi.
Kamanda Ngonyani Amewataja Watuhumiwa Wanne Waliokamatwa Na Silaha Aina Ya
Bastola Iliyotengenezwa Kyenyeji Na Risasi Mbili Za Bunduki aina ya Short Gun Na Wizi
Wa Mifugo Kuwa Ni Pamoja Na Shukrani Lugenge Mweye Umri Wa Miaka 42 ,Abdul
Kaduma Mwenye Miaka 38 ,Rashidi mguruni Mwenye Miaka 28 Na Gervas Muhuti
Mwenye Umri Wa Miaka 50 Wakazi Wa Katenge Na Maguvani Katika Halmashauri Ya
Mji Wa Makambako Mkoani Njombe.
SACP Ngonyani Amesema Watuhumiwa Wengine Waliokamatwa Na Mali Za
Wizi Ni Pamoja Na Salmu Hongori Mkazi Wa Mgendela,Peter Matola Na,Joshuwa
Mwalongo Wakazi Wa Mjimwema,Eva Kawogo Mkazi Wa
Nationalhousing ,Issa Shaban Mkazi Wa Uzunguni, Emili Mwalongo Mkazi Wa
Nazareth,Peter Luiva Mkazi Wa National Housing Na Salumu Kawogo Wote Wakazi Wa
Njombe Mjini.
Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Watuhumiwa Hao Wote Watafikishwa
Mahakamani Kujibu Tuhuma Zinazowakabili Ambapo Ametoa Wito Kwa Wananchi
Waliowahi Kuibiwa Kufika Katika Ofisi Za Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Ili Kuweza
Kutambua Mali Zao.
Wakizungumza Badhi Ya Wamiliki Waliofika Katika Ofisi Za Jeshi La Polisi Mkoa Wa
Njombe Kutambua Mali Walizowahi Kuibiwa Wamepongeza Jeshi Hilo Kwa Hatua Hiyo
Walioifanya Ya Kuwakamata Waharifu Na Mali Hizo Ambapo Wameomba Kuendelea Na
Kazi Hiyo Ili Kuweka Usalama Wa Mali Za Raia Huku Wengene Wakishindwa Kuziona
Mali Zao Walizo Wahi Kuibiwa Na Wengeine Wakifanikiwa Kuzitambua.
Zaidi Ya Mali 20 Zilizowahi Kuibiwa Kwa Wananchi Wa Maeneo Mbalimbali Mkoani
Njombe Zimepatikana Baada Ya Msako Mkali Ulioendeshwa Na Jeshi Hilo Zikiwemo
Silaha Aina Ya Bastola Na Risasi Za Bunduki aina ya Shorti Gun Ambapo Msako Huo
Bado Unaendelea Kuwabaini Majambazi Sugu Wengine Waliofanikiwa Kutoroka.
No comments:
Post a Comment