Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, October 2, 2014

WATU 20 WATIWA MBARONI LEO KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI MBALIMBALI MKOANI NJOMBE























Na Michael Ngilangwa Njombe

 Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Zaidi ya Watu 20 Wanaosadikiwa Kujihusisha na Vitendo Vya Wizi  Baada ya Kukamatwa na Mali Mbalimbali Zinazodhaniwa Kuwa za  Wizi.

Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema Watu Hao Wamekatwa Katika Oparesheni  Inayoendeshwa na Jeshi Hilo Kwa Mkoa wa Njombe.

Kamanda Ngonyani Amesema Jeshi Hilo Linaendelea na Oparesheni Hiyo Kwa Lengo la Kuwabaini Watu Wanaojihusisha Vitende Vya Uhalifu Pamoja na Kukomesha Vitendo Hivyo Ili Wananchi Waweze Kuendesha na Kuishi Kwa Amani, Kama Anavyoeleza.

Aidha SACP Ngonyani Amewaomba Wananchi Walioibiwa Mali Zao Kufika Katika Ofisi za Jeshi Hilo zaMkoa Ili Kutambua Mali Hizo Hapo Kesho Oktoba Tatu Kuanzia Majira ya Saa Nne Asubuhi.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limekuwa Likifanya Oparesheni za Kuwabaini Watu Wanaojihusisha na Vitendo Vya Uhalifu na Kuwafikisha Mahakamani.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa makosa mbalimbali na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamni kujibu tuhuma zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment