Baadhi ya waandishi wa habari wanaosafiri kwenda Malawi wakiwa wanamsikiliza Katibu tawala msaidizi wakati wa kuagana.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha akizungumza na waandishi wa Habari wanaotarajia kusafiri.
Mwenyekiti wa safari ya Malawi, Ulimboka Mwakilili, akitoa ufafanuzi wakati wa kuagana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Mwandishi Christopher Nyenyembe, mmoja wa Waandishi wanaosafiri akifafanua jambo.
Katibu tawala Msaidizi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Akiongea na Waandishi wa Habari wanaokwenda Safarini Malawi
Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro,
akiwasikiliza waandishi wa habari walipoenda kumuaga ofisini kwake.
baadhi
ya Waandishi wa Habari wakiwa ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Jiji la Mbeya wakimsikiliza kwa makini walipoenda kumuaga tayari kwa
safari ya Malawi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro akiwa katika picha
ya pamoja na waandishi wa habari wanaotarajia kusafiri baada ya kuagana.
BAADHI ya Waandishi
wa habari Mkoa wa Mbeya wanaotarajia kufanya ziara ya kimafunzo nchini
Malawi na Zambia wameagwa rasmi na viongozi wa Serikali.
Waandishi
hao wapatao 15 wanatarajia kuanza safari Septemba 14, Mwaka huu hivyo
kabla ya kuondoka wameagana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na
Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Maagano
hayo yamefanyika leo kwa nyakati tofauti na kupata Baraka zote kutoka
kwa wawakilishi wa Ofisi hizo na kuwataka waandishi kuuwakilisha vema
Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.
Katibu
Tawala Msaidizi, idara ya Utawala na rasilimali watu, Leonard Magacha,
kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, alisema
matarajio ya Mkoa ni kupata mrejesho kutoka kwa waandishi baada ya
kurudi kutoka safarini.
Alisema
hiyo ni fursa pekee ambayo waandishi wanaitumia kuvitangaza vivutio
mbali mbali vilivyopo katika Mkoa wa Mbeya kwa watu wa Malawi ili waweze
kutembelea pamoja na fursa zilizopo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk.
Samwel Lazaro, amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi hiyo
kuitangaza timu ya Mbeya City kimataifa zaidi.
Alisema
hivi sasa Halmashauri imekuwa na mahusiano mazuri na wananchi kutokana
na uwepo wa timu ya mpira wa miguu ambayo hivi sasa inajulikana nchi
nzima hivyo ni fursa iliyotokea ya kuitangaza nchi za Nje ili ijulikane
kimataifa zaidi.
Wakati
huo huo, Mwenyekiti wa Msafara wa Waandishi wa Habari kwenda nchini
Malawi, Ulimboka Mwakilili, ametoa shukrani kwa wadau mbali mbali
waliowezesha safari hiyo kwa hali na mali.
Alisema
mbali na kila mwandishi kuchangia gharama za kwenda na kurudi lakini
kuna wadau walioweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya safari
hiyo.
Aliwataja
baadhi ya wadau kuwa ni Mkurugenzi wa Hifadhi ya wanyama pori(Ifisi
Zoo), Leirner, WYCS, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ofisi ya Katibu
tawala Mkoa wa Mbeya, Faraja nursing na Maridadi Shop.
Aliongeza
kuwa wadau wengine wanakaribishwa kuchangia safari hiyo kutokana na
umuhimu wake katika kutangaza fursa ambazo zinapatikana katika Mkoa wa
Mbeya kwa wafanyabiashara na wananchi wa Nchi ya Malawi.
Naye
Mratibu wa Safari hiyo, Venance Matinya, alisema maandalizi ya safari
yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo kinachosubiriwa ni tarehe ya
kuondoka.
Alisema
waandishi wa habari wameshaajiandaa kwa mahitaji yote ya safari za nje
ya nchi ikiwa ni pamoja na kukata Hati za kudumu za kusafiria pamoja na
cheti cha chanjo ya ugonjwa wa manjano kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment