Balozi
wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa
Habari kutoka Mbeya walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi
Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi
Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Mkoani Mbeya wakimsikiliza Balozi kwa Makini
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akipokea Taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akijibu Taarifa ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya .
Waziri
wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa
akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri
wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa
Wa kwanza Kulia ni Afisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni akifuatilia Mkutano huo
Waandishi wa Habari wakiendelea kufuatilia Kikao hicho
Francis
Phiri wa kwanza Kulia ambaye ni Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na
Muasisi wa Nyika Press Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
Kikao kikiwa Kinaendelea
Waziri
wa Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa wa
pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi
wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya Ofisi yake Jijini Lilongwe.
Waziri wa Habari,Utalii na
Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa Kondwani Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya
Malawi haina mgogoro na Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.
Aliyasema hayo baada ya
kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini
kwake katika mfululizo wa ziara ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja
nchini humo katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.
Waziri Nankhumwa alisema kuwa Mtoto wa Rais wa Malawi Profesa Ather Muthalikana anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa
Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara
nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina yoyote ile itayowapelekea kuwagawa wananchi
wa pande hizo.
Aidha alisema kuwa ili kuonesha
hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa
kuchukua ndoano na kuvua samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia
kuwa wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi
wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa
mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.
Aliyasema hayo alipotembelewa
na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa
Tanzania nchini Malawi katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi
ili kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira,utalii
na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.
Balozi Tsere alisema hivi sasa
si wakati wa marumbano kwani inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza
baina ya viongozi wa nchi hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo
katika mahakama ya kimataifa ambapo
utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa mgogro huo.
Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi
hizo walifanya makubaliano ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa
ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama zilizopo
Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi
hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.
Katika ziara hiyo
Waandishi wa vyombo mbalimbali
walishiriki ikiwa ni pamoja na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira
na Raia Mwema.
Vingine na Tanzania
Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu Ulimboka Mwakilili ambaye alikuwa
Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa Ujenzi Claudio Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo
Na Mbeya Yetu Blog , Lilongwe Malawi.
No comments:
Post a Comment