NGUO NA MALI NYINGINE ZIMEUNGUA NA MOTO HUO
HIKI NI CHUMBA AMBACHO MALI ZIMETEKETEA KWA MOTO BAADA YA SHOTI YA UMEME KUTOKEA NA MOTO HUO KUUNGUZA MALI HIZO
HAWA NI BAADHI YA MASHUHUDA WALIOKUWEPO HUKU BAADHI WAKIONEKANA KUIKIMBIA KAMERA NA KUFICHA NYUSO ZAO ZISIONEKANE
VIONGOZI WA MTAA WAKIANGALIA JINSI ILIVYOKUWA CHUMBANI MOTO ULIKOTOKEA
HUYU NI MWENYEKITI WA MTAA WA MPECHI SALOME MDEM AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOKUWEPO
VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA WAKIINGIA KUANGALIA ATHALI ZILIZOMKUTA MFANYAKAZI WAO AMBAYE AMEUNGULIWA NA MALI ZAKE
Na Michael Ngilangwa-Njombe
Moto Mkubwa umeibuka na kuteketeza baadhi ya mali za mkazi mmoja wa mtaa wa Mpechi Bi.Enea Mgaya Ambaye ni mfanyakazi wa ofisi ya Chama cha mapinduzi Wilaya ya Njombe uliotokea leo majira ya saa saba mchana wakati wamiliki wa nyumba hiyo wakiwa hawapo.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema Chanzo cha moto huo huenda ni shoti ya umeme Ambapo wamesema ukweli zaidi unaendelea kuchunguzwa na vyombo vya usalama.
Aidha Wananchi hao wameshukuru jitihada za kufanikisha kuokoa baadhi ya mali ndani ya nyumba hiyo Na kwamba jitihada hizo zinapaswa kuendelezwa hata maeneo mengine pindi msaada unapohitajika Huku mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika, akiwa eneo la tukio hilo akitaka taarifa zisichukuliwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu zake binafsi.
Akizungumza na Mtandao huu Msimamizi wa nyumba hiyo bwana Isack Mlowe ameshukuru wananchi kwa jitihada walizoonesha katika tukio hilo na kwamba chanzo halisi hakijafahamika Ambapo imedaiwa kuwa huenda tukio hilo likahusishwa na shoti ya umeme.
michaelngilangwa.blogspot.com wa Mtandao huu iliutafuta Uongozi wa mtaa huo Akiwemo Afisa mtendaji Isabela Malangalila na mwenyekiti wake Salome Mdem Ambao wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo chake huku jitihada za kusaidia wahanga hao zikiendelea.
Hata hivyo viongozi hao wamewatupia lawama wananchi na barozi wa eneo hilo kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa mtaa jambo Ambalo wameahidi kutoa elimu ya utawala bora kwenye mikutano ya hadhara kuhusiana na mabarozi kutoa taarifa za matukio yakiwemo ya wizi na moto .
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ya Njombe Clemence Mponji Akiwa eneo la Tukio amesema wasamalia na wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia wahanga hao kwa msaada wowote wakati wahanga wakiendelea na jitihada za kutafuta mali nyingine .
No comments:
Post a Comment