SHIRIKA LA SHIPO LATAMBULISHA MRADI WA SHULE YA CHEKECHEA JOSHONI NJOMBE
WANANCHI WA MTAA WA JOSHONI WAKIWA KATIKA MAKUNDI YA MAJADILIANO KATIKA OFISI YA MTAA HUO
DIWANI WA KATA YA MJIMWEMA AKIWAELEKEZA WANANCHI NA KUWAPANGA KATIKA MAKUNDI KUJADILI MRADI HUO WA UJENZI WA CHEKECHEA HIYO
Na Erasto Mgeni Njombe
Katika
Kuhakikisha Miradi Mbalimbali Inatekelezwa Kupitia Asasi Zisizo za
Kiserikali Mkoani Njombe,Mashirika Hayo Yameonekana Kuongeza Kasi Ya
Kutekeleza Miradi Yao Kama Wajibu Wao Kwa Kushirikiana na Serikali.
Aidha
Shirika Lisilo la Kiserika la SHIPO Lililopo Mkoani Njombe Hii Leo
Limetambulisha Rasmi Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Chekechea Ambao
Unatarajiwa Kujengwa Katika Mtaa wa Joshoni Kwa Kushirikiana na Wananchi
wa Mtaa Huo.
Akitambulisha Mradi wa Ujenzi Huo Katika Ofisi za
Mtaa wa Joshoni Mjini Njombe Mmoja wa Viongozi Kutoka SHIPO Bonaventura
Mdamu Amesema Mradi Huo wa Ujenzi Utahusisha Vyumba Viwili Vya Madarasa
na Ofisi za Walimu .
Bwana Mdamu Ameongeza Kuwa SHIPO Ilikuwa na
Mpango wa Ujenzi wa Shule ya Awali Katika Mtaa Huo Tangu Mwaka 2011
Huku Akiwaomba Wakazi wa Mtaa Huo Kutoa Ushirikiano Ili Kukamilisha
Haraka Mradi Huo.
Jimmy Ngumbuke ni Diwani wa Kata ya Mjimwema
Mjini Njombe Ambaye Amelishukuru Shirika Hilo na Kuuhakikishia Uongozi
wa SHIPO Kuwa Wakazi wa Mtaa Huo Watashiriki Katika Mradi Huo Hadi Hapo Utakapokakamilika , Huku Afisa
Mtendaji
wa Mtaa wa Joshoni Isabela Malangalila Akiuomba Uonngozi wa Halmashauri
ya Mji wa Njombe Kutoa Ushirikiano wa Miradi Inayotkelezwa Katika Mtaa
Huo.
Shirika la SHIPO Limekuwa Likichangia Maendeleo Katika Sekta Mbalimbali Mkoani Njombe Hususani Katika Huduma za Kijamii.
No comments:
Post a Comment