Friday, April 11, 2014
MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA ELIMU
WANAFUNZI WA KUTOKA SHULE MBALIMBALI ZA MSINGI NA SEKONDARI WILAYANI MAKETE AMBAKO MAADHIMISHO HAYO YAMEFANYIKIA LEO
MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIKABIDHI VYETI KWA WAKUU WA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI MWAKA 2013
KUNDI LA SANAA ZA MAONESHO LA SUMASESU LIKIFANYA MAONESHO MBELE YA UMATI WA WALIOHUDHURIA MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA ELIMU
MKUU WA MKOA WA NJOMBE WA TATU KUTOKA UPANDE WA KULIA ,NA WA PILI KUTOKA UPANDE WA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA MAKETE JOSEPHINE MATIRO NA WA KWANZA TOKA UPANDE WA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA WAKIWA NA MAAFISA MBALIMBALI WA ELIMU MKOA NA WILAYA.
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi Amewaagiza Wadau Wa Elimu Mkoani Hapa Kuwajibika Kila Mmoja Kwa Nafasi Yake Ili Kufanikisha Utekelezaji wa Agizo la Serikali la Matokeo Makubwa Sasa.
Capteni Mstaafu Asseri Msangi Ametoa Agizo Hilo Hapo Jana Wilayani Makete Mkoani Hapa Katika Maadhimisho Ya Wiki Ya Elimu Yaliyofanyika Wilayani Humo Kimkoa Na Kusema Kwamba Ushirikiano Wa Pamoja Kila Mtu Kwa Nafasi Yake Kutasaidia Kuzidi Kuinua Kiwango Cha Elimu Mkoani Njombe.
Msangi Amesema Suala La Kuongeza Kiwango Cha Ufaulu Ni La Kila Mmoja Hivyo Amewaagiza Maofisa Elimu wa Wilaya Zote za Mkoa wa Njombe Kupita Kwenye Kila Shule Za Sekondari Na Msingi Kubaini Changamoto Zinazosababisha Wanafunzi Kufanya Vibaya Kwenye Mitihani Yao.
Amesema Jumla Ya Wanafunzi 538 Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza Mwaka Huu Bado Hawajaripoti Shuleni na Hivyo Ametoa Agizo Kuwa Wanafunzi Hao Watafutwe Popote Walipo Ili Waripoti Shuleni Tayari Kwa Masomo.
Awali Akisoma Risala Kwa Niaba Ya Wanafunzi Wenzake Mkoani Njombe, Noela Msinangila Amesema Licha ya Serikali Kuongeza Jitihada za Kuongeza Miundombinu ya Elimu Lakini Bado Inapaswa Kuendelea Kutatua Changamoto Zinazowakabili Ikiwemo Uhaba Wa Vyumba Vya Madarasa.
Kwa Upande Wake Afisa Elimu Mkoa Wa Njombe Bwana Said Nyasiro Amesema Mkoa Wa Njombe Umejipanga Vilivyo Katika Kuinua Kiwango Cha Elimu Siku Hadi Siku Kulingana Na Mipango Iliyowekwa Ikiwemo Kuhakikisha Wanafunzi Wanasomea Katika Mazingira Mazuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment