WA KWANZA UPANDE WA KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAULO MALALA,WA PILI KUTOKA KULIA NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSATAAFU ASERI MSANGI,WA TATU NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENCE KABELEGE NA WA NNE NI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAU
WAKUU WA IDARA MBALIMBALI TOKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAKIWA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI HIYO
AFISA HABARI MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA PHILEMON
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIWASILI KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
AFISA HABARI WILAYA YA NJOMBE LUKERO MSHAULA AKISIKILIZA KWA UMAKINI MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI
MUHANDISI WA MAMLKA YA MAJI WILAYA YA NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Captain msataafu Aseri msangi amepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya halmashauri Na za wakuu idara Wilaya ya Njombe taarifa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo bwana Paulo Malala mapema leo katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Akiwasilisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe bwana Pulo Malala amesema halmashauri imeendelea kuwezesha vikundi vya vijana na wanawake ili wajikwamu na dimbwi la umasikini ambapo kwa kipindi cha mwaka 2012 na 2013 halmashauri ilitoa jumla ya shilingi milioni ishilini na nne kama mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi 24 vya wanawake.
Aidha bwana Malala amesema kuwa kati ya shilingi milioni ishilini na nne zilizotengwa kwa kipindi cha mwaka 2012 na 2013 shilingi milioni kumi na moja zilitengwa kwaajili ya vijana ambapo katika kipindi cha mwezi julai 2013 hadi machi 2014 halmashauri ya wilaya imeendelea na mchakato wa kuviandaa vikundi vya wanawake na vijana 32 kwaajili ya kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni ishilini na nne.
Katika taarifa ya fedha iliyosomwa na mkuu wa Idara ya fedha Rhoda Mahava imeeleza mikakati mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo ikiwemo halmashauri kufanya mapitio katika kipindi cha mwezi april hadi june 2014 ,Halmashauri imebinafsisha ukusanyaji wa mapato katika kata ya Ikuna huku mchakato wa kubinafsisha magulio ya Kidegembye,Mtwango,Matembwe na Ikondo unaendelea.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya kwanza iliowasilishwa na idara ya Fedha mkuu wa mkoa wa Njombe Aseri Msangi amezitaka halmashauri kuweka mipango mikakati dhabiti ya ukusanyaji wa mapato ambapo wahusika wa kusimamia ukusanyaji huo ni watendaji wa vijiji.
Amesema kuwa ni vema halmashauri za wilaya zihakikishe watendaji wote wa vijiji na kata wanaishi karibu na mahala pa kazi ili kurahisisha ukusanyaji mapato kwa urahisi zaidi na kwamba mkoa wa Njombe watendaji wengi hawaishi katika maeneo yao ya kazi.
No comments:
Post a Comment