Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, April 12, 2014

DIWANI WA KATA YA RAMADHANI ALFRED LUVANDA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA MITAA YA KATA HIYO





DIWANI WA KATA YA RAMADHANI ALFRED LUVANDA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MTAA WA WIKICHI



WANANCHI WA MTAA WA WIKICHI WAKISIKILZA KWA MAKINI DIWANI HUYO




HUYU NI MWENYEKITI WA MTAA WA WIKICHI BWANA DANIEL MTWEVE AKIJIBIA BAADHI YA HOJA ZILIZOIBULIWA NA  WANANCHI


HUYU NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA RAMADHANI BWANA  KENETH MHEPELA AMESEMA MARUFUKU MWENYEKITI KUCHUKUA NA KUHIFADHI FEDHA ZA WANANCHI MWENYE JUKUMU HILO NI AFISA MTENDAJI WA MTAA HUSIKA




BAADA YA MKUTANO KUMALIZIKA WANANCHI SASA WANATAWANYIKA KWENDA KWENYE SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.


Viongozi wa serikali za mitaa kata ya Ramadhani wametakiwa kufungua akaunt za ofisi za mitaa yao ili kuepukana na upotevu wa fedha za michango ya wananchi ambayo wanachangia kwaajili ya kutekeleza miradi pamoja na mitaa hiyo kurudishiwa asilimia kumi kutoka halmashauri ya mji wa Njombe.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa kata ya Ramadhani Alfred Luvanda wakati akiwa kwenye ziara yake ya kukagua na kuwasikiliza wananchi changamoto zinazowakabili ambapo amebaini kuwepo kwa mapungufu kwa baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa na kuwataka kurekebisha tofauti zao ili kupunguza migogoro baina yao na wananchi kwa kuhakikisha wanafanikisha zoezi la kufungua akaunti benki na kuhifadhi michango ya fedha hizo.

Akiwa katika mtaa wa Wikichi diwani Luvanda amepokea malalamiko  kutoka kwa wananchi Ya kwamba ofisi ya mtaa haina akaunti benki  ya kuhifadhi pesa za michango   ,mgogoro wa mpaka kati ya mtaa huo na mtaa wa mgodechi  na kutozwa faini kubwa na viongozi wa baraza la kata jambo ambalo ni kero kwao huku makubaliano ya diwani na wananchi wa mtaa huo  wakimteua  Thomas Mgimba kuwa kaimu mtendaji  wa mtaa huo ambapo baadhi ya changamoto akichukua na kuahidi kwenda kuzitafutia ufumbuzi .

Akizungumza  kwenye mkutano wa hadhara mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Ramadhani bwana Keneth Mhepela amepiga marufuku kwa kiongozi yeyote aliechaguliwa kupitia chama cha mapinduzi kushika fedha za wananchi na kwamba mwenye mamlaka ya kushika na kukusanya fedha hizo ni afisa mtendaji wa mtaa husika huku akiahidi kufuatilia kila mtaa ili kubaini tatizo la wenyeviti kukusanya na kukaa na fedha za wananchi kinyume na sheria.

Mwenyekiti wa mtaa wa Wikichi Bwana Daniel Mtweve akajibia baadhi ya changamoto ambazo zililalamikiwa na wananchi wa mtaa huo huku akisema mgogoro wa mpaka kati ya mgodechi na Wikich ukifanikiwa kupatiwa ufumbuzi.

Awali wakihoji maswali wananchi wa mtaa wa Wikichi wamelalamikia mambo mbalimbali ikiwemo afisa mtendaji wa mtaa huo kusimamia mitaa mingi,darasa la chekechea kutokamilika ikiwa lilianza kujengwa kwa muda mrefu licha ya wananchi kuchangia fedha, baraza la usuruhishi la kata ya Ramadhani kutotenda haki kwa wananchi huku wakimshukuru diwani kwa kufika na kuwasikiliza changamoto zinazowakabili na kwamba changamoto zote zimeanza kujitokeza baada ya diwani huyo kwenda kupatiwa matibabu.


No comments:

Post a Comment