Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, November 21, 2013

WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA MBALIMBALI LIKIWEMO LA MAUAJI YA MTOT0 WA MIEZI SITA ALIYELALIWA NA WAZAZI WAKE WILAYANI LUDEWA KUTOKANA NA ULEVI WA POMBE

 AFISA MNADHIMU WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE FOCUS  MALENGO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO OFISINI KWAKE


Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe akiwemo   mkazi mmoja wa kijiji cha Witili kata ya Lupanga taarafa ya mlangali Timoth Mgimba  26 wilayani Ludewa  anaeshikiliwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mtoto wake mwenye umri wa miezi sita aliyeuwawa baada ya kulaliwa na wazazi hao.

Akizungumza na kituo hiki Afisa mnadhimu wa jeshi  la polisi mkoa wa Njombe Focus Malengo amesema kuwa katika tukio hilo limetokea november 20 mwaka huu ambapo katika tukio hilo anashikiliwa mtuhumiwa mmoja ambae  ni Timoth Mgimba huku mama na mtoto huyo akitokomea kusiko julikana.

Aidha kamanda malengo ameyataja matukio mengine kuwa ni pamoja na tukio la wizi wa mifugo aina ya kondoo mali ya Joasisi Nasi mkazi wa  kijiji cha Luwanda  mwenye thamani ya shilingi elfu tisini ambapo watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi  Idd Wasara 22 na Oscar Gala wote wakazi wa kijiji cha Igeleheja na kwamba  Mtuhumiwa Oscar Gala amelazwa katika hospitali ya Ilembula kwa matibabu baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali tukio walilolifanya november november 20 majira ya saa kumi nambili asubuhi .

Kamanda Malengo amesema kuwa tukio lingine mkazi wa kijiji cha  Utengule wilayani Njombe Mayale Wandu 28 aliuwawa na watu wasiyofahamika kwa kukatwa katwa na kitu chenye ncha kali kichwani ambapo mpaka sasa jeshi la polisi linawashikiliwa watu wawili kwa uchunguzi ambao ni Paulo Elias 26 na Dan 41 wote wakazi wa kijiji cha     Utengule wilayani Njombe na kwamba mwili wa marehemu ulikutwa ndani ya nyumba yake ukiwa umeharibika katika tukio lililogundulika november 20 majira ya saa mbili asubuhi.

Hata hivyo kamanda huyo amesema tukio lingine mkazi mmoja wa Igominyi Frola Chengula alikutwa akiwa amefariki dunia baada ya kuangukiwa na mti na kisha kufariki dunia ambapo uchunguzi wa awali wa  jeshi la polisi umebaini kuwa marehemu alikuwa na matatizo ya akili katika tukio liligundulika mnamo november 18 mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment