MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA POLINI KANDO KIDOGO NA BARABARA YA KUELEKEA KIJIJI CHA YAKOBI KARIBU NA NYUMBANI KWAO HUKU PIKIPIKI YAKE IKISADIKIKA KUCHUKULIWA NA WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO AMBAO HAWAKUJULIKANA
HAWA NI WENZAKE NA MAREHEMU AMBAE ALIKUWA AKIFANYA KAZI ZA KUSAFIRISHA ABIRIA KWA KUTUMIA USAFIRI WA BODABODA KATIKA KIJIWE CHA SANGAMELA MJINI NJOMBE NA HAPA WANAJADILI NAMNA YA KUJIHAMI NA MAADUI WANAOSABABISHA VITENDO HIVYO VYA UPOLWAJI WA PIKIPIKI.
Baadhi ya Wamiliki na Madereva wa Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Mjini Njombe Wameandamana Hadi Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Njombe Wakilaani Kitendo cha Mauwaji na Vitendo Vya Utekaji Nyara Madereva Hao Vinavyofanywa na Watu Wanaosadikiwa Kuwa ni Majambazi
Aidha Wamiliki na Madereva wa Pikipiki Pia Wamelalamikia Kitendo cha Jeshi la Polisi Kutofika Kwa Wakati Eneo la Tukio Licha ya Kupewa Taarifa Mapema.
Wamiliki na Madereva wa Pikipiki Hao Wamefanya Maandamano Hayo Kufuatia Mauwaji ya Dereva Pikipiki Enock Kihindo Aliyekodiwa Siku ya Jumapili Kutoka Kituo cha Sangamela Kwenda Kijiji cha Yakobi, Ambaye Mwili Wake Umekutwa Porini Barabara Yakuelekea Yakobi ,Huku Mikoni
Akielezea Sababu za Kuchelewa Kufika Katika Eneo la Tukio Kamanda wa Polisi Wilaya ya Njombe OCD Lucy Mwakafwila Amesema ni Kutokana na Kufanya Maandalizi Kuelekea Eneo Hilo la Tukio Pamoja na Kumsubiri Daktari wa Hospitali ya Wilaya Kwa Ajili ya Uchunguzi wa Mwili Huo.
Marehemu Enock Kihindo Alipotea Katika Mazingira ya Kutatanisha Siku ya Jumapili Novemba 10 Mwaka Huu Baada ya Kukodiwa na Mtu Aliyetaka Kumpeleka Maeneo ya Yakobi , Huku Jitihada za Kumtafuta Zikiendelea Baada ya Kutoonekana Kituo Chake cha Kazi Hadi Hii Leo Walipouona Mwili Wake Ukiwa Umetupwa Porini.
Mwili wa Marehemu Enock Kihindo Umezikwa Leo Katika Kijiji cha Lwangu Kata ya Kifanya Baada ya Kukamilika Kwa Taratibu Zote.
No comments:
Post a Comment