Thursday, October 10, 2013
TIMU YA POLISI NJOMBE LEO IMEKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO TOKA KAMPUNI YA DAR CHAINSAWS AGENCIES TOKA DAR ES SALAAM
TIMU YA POLISI NJOMBE WAKISHUHUDIA KUKABIDHIWA VIFAA HIVYO VYA MICHEZO
AKIKABIDHIWA VIFAA HIVYO KAMANDA WA POLISI ACP FULGENCE NGONYANI ASUBUHI YA LEO
BWANA MWAINSASU AKIKABIDHI JEZI KWA KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE
Kampuni ya biashara ya Dar Chainsaws Agencies kutoka Dar es Salaam leo imekabidhi
vifaa vya michezo kwa timu ya polisi ya mkoa wa Njombe vyenye thamani ya shilingi
milioni tano ambapo pamoja na mambo mengine wachezaji wametakiwa kujikita zaidi
katika kuboresha kiwango cha michezo na kutambua kuwa michezo ni ajira.
Vifaa vilivyokabidhiwa na Kampuni hiyo ni pamoja na jez seti tisa,mipira kumi na
mbili,bips za mazoezi 25 vyote vikiwa na jumla ya shilingi milioni tano.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya mkurugenzi wa Kampuni hiyo
,afisa masoko kutoka kampuni ya biashara ya Dar Chainsaws Agencies bwana Greyhpord
Mwansasu maarufu kwa jina la IPINDA amesema kuwa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo ni la
mwendelezo na kwamba kampuni hiyo ipo tayari kutoa vifaa hivyo kwa timu
itakayoonesha moyo wa kushiriki michezo kikamilifu itaweza kusaidiwa vifaa mbalimbali
vya michezo toka kwa kampuni hiyo.
Aidha bwana Mwainsasu amesema kuwa siku chache zilizopita kampuni hiyo ilifanikiwa
kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Njombe United vifaa vyenye thamani ya shilingi
milioni moja na laki tano zoezi lililofanyika mnamo september 15 mwaka huu.
Amesema kuwa kampuni hiyo bado inaendelea na udhamini zaidi kwa michezo
mbalimbali inayoendelea kufanyika mkoa wa Njombe huku akiwataka vijana kushiriki
michezo hiyo kwa wingi ili kupunguza idadi ya wazururaji na vibaka.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo vya michezo toka kwa kampuni ya Dar C
hainsawes kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani
ameishukuru kampuni hiyo kwa kusaidia vifaa hivyo katika timu zinazoshiriki ligi daraja la
mkoa na kwamba kampuni hiyo iliweza kuwaahidi kuwapatia na hatimae leo
wamekabidhiwa.
Aidha kamanda Ngonyani amesema kuwa anatoa wito kwa wadau wengine kujitokeza
kuisaidia timu ya polisi Njombe ili iweze kusonga mbele huku akiwaasa wachezaji wa timu
hiyo kuwa msaada huyo walioupata uwe moja ya kivutio kwa wengine kwa kumuunga
mkono kuonesha matunda yanayotarajiwa kwa kuonesha kiwango katika michezo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment