HILI NDILO GARI ALILOLIKABIDHI LEO KWA MKUU WA MKOA WA NJOMBE
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIWA NDANI YA GARI AKIJARIBU KULIWASHA GARI HILO
NAIBU WAZIRI WA MAJI BINILITH MAHENGE AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA MKOA WA NJOMBE
Serikali Imetenga Kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5 Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha
2013 / 2014 Kwa Ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maji Katika Halmashauri ya Mji
wa Njombe.
Kauli Hiyo ya Serikali Imetolea Leo na Naibu Waziri wa Maji Dkt. Binilith Mahenge
Wakati Akikabidhi Gari Kwa Ajili ya Idara ya Maji Mkoa wa Njombe Kwa Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Keptein Mstaafu wa Aseri Msangi na Kusema Kuwa Fedha Hizo
Zilizotengwa Zitatumika Katika Miradi ya Maji Inayotekelezwa Katika Halmashauri
ya Mji wa Njombe.
Aidha Naibu Waziri Mahenge Amemtaka Mhandisi wa Maji Mkoa wa Njombe
Kuhakikisha Anafuatilia Utekelezaji wa Miradi Yote ya Maji na Kubaini Changamoto
ya Maji Zinazoyakabili Baadhi ya Maeneo Hasa Vijijini.
Halikadhalika Naibu Waziri Huyo wa Maji Amesema Miradi Mingi Imekuwa
Ikitekelezwa Chini ya Kiwango Kutokana na Wahandisi wa Mikoa na Wilaya
Kutofauatilia Kwa Ukaribu Utekelezaji wa Miradi Hiyo.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Mkoa Keptein Mstaafu Aseri Msangi Amemuhakikishia
Naibu Waziri Huyo Kufuatilia Miradi Yote ya Maji Inayotekelezwa Mkoani Njombe
Kuhakikisha Inakamilika Ifikapo Juni Mwaka 2014 Huku Akiahidi Kuwachukulia
Hatua za Kisheria Kwa Watumishi na Wakandarasi Watakaoshindwa Kukamilisha
Miradi Hiyo Kwa Wakati
Akizungumza Mara Baada ya Kukamilika Kwa Zoezi la Kukabidhi Gari Hilo Mhandisi
wa Maji Mkoa wa Njombe Christopha Nyandiga Amesema Mradi wa Maji Kutoka
Chanzo cha Mto Nyenga Zinaendelea Zikiwa Katika Hatua za Tathimini
Jumla ya Miradi Kumi Inatekelezwa Kwa Kila Wilaya za Mkoa wa Njombe Huku
Miradi Mitano Ikitarajia Kukamilika Mwaka Huu.
No comments:
Post a Comment