Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, September 6, 2013

WANANCHI BLOCK X WALIA NA MIUNDOMBINU DUNI YA BARABARA,WATAKA KUKATISHA UWANJA WA NDEGE

Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Lupyana Fute Ametembelea Uwanja wa Ndege wa Mjini Njombe na Kukagua Baadhi ya Maeneo ya Uwanja Huo na Kujionea Uharibifu Uliofanyika Katika Uwanja Huo Kutokana na Shughuli Mbalimbali za Wananchi.

Aidha Diwani Fute Amehoji Kuhusu Suala la Walinzi wa Uwanja Huo  Kuwatoza Faini Wananchi Wanaokiuka Sheria za Uwanja Huo Bila Kuwapa Stakabadhi za Malipo, Huku Akiwataka Wananchi Kufuata Taratibu za Uwanja Huo.

Kuhusu Miundombinu ya Barabara Kwa Wananchi wa Eneo la Block X Diwani Fute Amewaomba Wananchi wa Eneo Hilo Kuwa na Subira  Wakati Serikali Ikijiandaa Kukarabati Barabara Hizo na Kuendelea Kuitumia Barabara Iliyopo Kwa Sasa.

Diwani Fute Ameutaka Uomgozi wa Uwanja Huo Kutoa Elimu Kwa Wananchi Kuhusiana na Taratibu na Sheria za Viwanja Vya Ndege Kabla ya Kuwachukulia Hatua za Kisheria.

Kwa Upande Wake Msimamizi wa Uwanja Huo Benedict Nkonjera Amekanusha Suala la  Wananchi Wanaopita Katika Uwanja wa Ndege  Kuwatoza Faini na Walinzi wa Uwanja Huo.

Kumekuwepo na Malalamiko Mbalimbali Kutoka Kwa Wananchi Juu ya Kutozwa Shilingi Elfu 20 Kama Faini na Walinzi wa Uwanja Huo Pindi Wanapopita Kwenye Uwanja wa Ndege.

Kwa upande wao Wananchi wa mtaa wa Kampalage katika eneo la block x mjini Njombe wamelalamikia  serikali kwa kushindwa kuwatatulia baadhi ya changamoto zinazowakabili  kwa muda mrefu ambapo pamoja na mambo mengine wamesema kuwa hali hiyo inasababisha kurudisha nyuma uchumi  na utendaji kazi kwa wananchi hao.

Miongoni mwa mambo wanayolalamikia wananchi hao ni pamoja na miundombinu duni ya barabara,kukamatwa na askali mgambo wanaolinda uwanja wa ndege na kuchukua fedha shilingi elfu ishilini pasipo kuwakatia risiti pindi wanapokatisha kwenye uwanja wa ndege ambapo katika kutatua hilo wameomba serikali iweke njia maalumu katika uwanja huo ili waweze kuitumia wananchi na wanafunzi wanapokwenda kupata mahitaji ya shule na nyumbani mjini Njombe.

Aidha wananchi hao wakizungumza mbele ya afisa mtendaji wa kata ya Njombe Mjini Donald Mng'ong'o wamesema kuwa endapo serikali haitochukua hatua za haraka kuwatatulia changamoto ya kukatisha kwenye uwanja huo wataendelea kupita kwenye uwanja huo  na kutishia kuchukua hatua zozote dhidi ya walinzi wa uwanja wa ndege ambao wamedaiwa kuwanyanyasa wananchi hao.

Hata hivyo wananchi hao wamesema kuwa mahitaji mengi muhimu ya kijamii ikiwemo shule,na masoko yanapatikana upande wa pili wa uwanja wa ndege jambo linalowalazimu kukatisha kwenye uwanja huo kwa kuwa sehemu wanayoelekezwa kupita ni ya mzunguko mkubwa hali ambayo inapelekea wanafunzi,watumishi na watu wa kawaida kuchelewa kwenye vituo vyao vya kazi na shuleni na kuamua kupita katikati ya uwanja ambapo serikali inatakiwa kujenga uwanja huo kwa kiwango cha lami na kuwatengea njia ya kupita kwa kukatisha kwenye uwanja huo.

Donald Mng'ong'o ni afisa mtendaji wa kata ya Njombe mjini  amesema kuwa kwa sasa haruhusiwi kupita mtu yeyote kwenye uwanja huo kwa kuwa sheria ya usafili wa anga hairuhusu na kuwataka wawe na subira mpaka miundomabinu na mbinu nyingine za kiserikali zitakapofanyika.

Aidha bwana Mng'ong'o amesema  serikali ipo kwenye mpango wa kuukarabati uwanja huo kwa kujenga uzio kuzunguka uwanja wote huku akiwapongeza wananchi wa uamuzi wao wa kusema wapo tayari kuchangia pesa kwaajili ya kujenga njia za kupita katika ya uwanja huo kwa kiwango cha lami endapo serikali itaridhia wafanya hivyo.

No comments:

Post a Comment