Tuesday, September 17, 2013
HALMASHURI YA MJI WA NJOMBE YAZIDIWA NA TATIZO LA TAKA KWENYE VIZIMBA
HAPA NI ENEO LA SOKO KUU LA NJOMBE MJINI SEHEMU YAKUMWAGA MAJI MACHAFU YAFURIKA MPAKA NJE HARUFU CHAFU YAWAKUTA WAFANYABIASHARA WA ENEO HILO
NYUMA YA KITUO KIKUU CHA MABASI NJOMBE TAKA ZA JAA KWENYE KIZIMBA NI KARIBU KILA SIKU ZOTE
HAPA NI MTAA WA POSTA KATI AMBAPO WANANCHI WALILALAMIKIA KUTOZOLEWA TAKA KWENYE VIZIMBA VYA MTAA HUO KWA ZAIDI YA MIEZI MITATU
BADO NI MTAA WA POSTA NA HAPA WAAMUA KUCHOMEA KWENYE KIZIMBA HAPOHAPO BAADA YA KUONA WAZOAJI TAKA HIZO HAWAPO
Serikali ya Mtaa wa Posta Kati Mjini Njombe na Wananchi wa Mtaa Huo Wamekubaliana Kuanza Ujenzi wa Ofisi ya Mtaa Huo Inayotarajia Kugharimu Shilingi Milioni 27 Hadi Kukamilika Kwake.
Aidha Katika Mkutano wa Hadhara Uliofanyika Jana Kwa Ajili ya Kusoma Taarifa ya Hesabu za Mapato na Matumizi Wananchi wa Mtaa wa Posta Kati Wamekubaliana Kuchangia Shilingi Elfu 30 Kila Mwananchi Mwenye Uwezo wa Kufanyakazi.
Akiongea Kwenye Mkutano Huo Mwenyekiti wa Mtaa Posta Kati Astasasta Kibangali Amesema Wananchi Hao Watachangia Fedha Hizo Kwa Awamu na Kwamba Unatarajia Kuanza Mara Baada ya Michango Kukamilika na Kuwataka Wananchi Kuchangia Michango Hiyo Mapema Ili Kuharakisha Ujenzi Huo.
Awali Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Wananchi wa Mtaa wa Posta Kati Wameiomba Serikali ya Mtaa Huo Kujenga Daraja Linaliunganisha Mtaa Huo na Mtaa wa Matalawe Ili Kuondoa Usumbufu Kwa Wananchi wa Mitaa Hiyo Kipindi cha Masika.
Katika Hatua Nyingine Wananchi Hao Wamependekeza Faini Zinazolipwa na Watu Mbalimbali Ikiwemo Wasiotoa Michango Kwa Hiari Zisimamiwe na Viongozi wa Mtaa Ili Zisaidie Katika Shughuli za Maendeleo
...................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment