Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, September 16, 2013

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA NJOMBE CHA KAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI MKUU

Halmashauri ya Mji wa Njombe Imekiri Kuwepo Kwa Baadhi ya Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi ya Ujenzi Chini ya Kiwango Ikiwemo Miradi ya Ujenzi wa Barabara na Kupelekea Barabara Hizo Kutumika Muda Mfupi na Kisha Kuharibika.

Akiongea Kwenye Kikao cha Viongozi wa CCM Kata ya Kifanya na Serikali ya Kata Hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edwin Mwanzinga Amesema Baadhi ya Wakandarasi Wanatekeleza Miradi Hiyo  chini ya Kiwango na Kuitia Hasara Serikali Huku Akiahidi Kulifanyia Kazi Suala Hilo.

Amezitaja Baadhi ya Barabara Zilizojengwa Chini ya Kiwango Kuwa ni Pamoja na Barabara ya Lwangu- Utengule na Kusema Kuwa Ujenzi wa Daraja Katika Barabara Hiyo  Litajengwa Hivi Karibuni

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Adam Msigwa
Amewataka Viongozi wa Vijiji na Kata Kuhakikisha Wanasimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 / 2015.

Awali Akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali Inayotekelezwa Kwenye Kata Hiyo Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kifanya Ditrick Danda Amesema Ili Kutekeleza Sera ya Utunzaji wa Mazingira, Zaidi ya Miti Milioni Tatu Imepandwa Katika Kipindi cha Mwaka wa 2012/2013.

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa wa wilaya ya Njombe Lupyana Fute hapa akazungumza baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kata hiyo na kuwataka wananchi kuepukana na tabia ya uchochezi wa migogoro ya kidini,kikabila na kisiasa miongoni mwao badala yake wafanye kazi kwa manufaa yao na taifa zima.
Chama cha mapinduzi wilaya ya Njombe jana kimekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010/2015 kwa kutembelea ujenzi wa miradi ya nyumba ya mtumishi wa afya katika zahanati ya kijiji cha Utengule,ujenzi wa barabara ya kutoka kijiji cha lwangu hadi Utengule,kituo cha wanyama kazi kilichopo kata ya kifanya na  baadae kufanya kikao cha ndani na wanachama wake katika makao makuu ya kata hiyo ya kifanya.


No comments:

Post a Comment