Wednesday, July 24, 2013
ZAHANATI YA KIJIJI CHA IKONDO WILAYANI NJOMBE IMEFUNGWA KUTOKANA NA WAUGUZI KWENDA KWENYE SEMINA ....
TAARIFA YA KATA YA IKONDO ILIYOSOMWA NA AFISA MTENDAJI WA KATA HIYO
Zahanati ya Kijiji cha Ikondo katika kata ya Ikonda
wilayani Njombe imesimama kufanya kazi kwa muda wa siku ya mbili
sasa baada ya wauguzi na wakunga wa zahanati hiyo kufunga na kwenda
kwenye semina mjini Njombe ambapo pamoja na mambo mengine wagonjwa
wa kijiji hicho wapo hatarini kupoteza maisha kwa kukosa huduma za
matibabu.
Wakizungumza Mbele ya Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Bwana Deo
Sanga wananchi wa kijiji cha Ikondo wamelalamikia kufungwa kwa
zahanati hiyo kutokana na kile kilicho daiwa kuwa madaktari
wamekwenda kwenye semina tangu jana 23 huku wagonjwa wakiachwa
pasipo kupatiwa huduma za matibabu.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa katika zahanati hiyo wanakabiliwa
na changamoto mbali,mbali ikiwemo ya ukosefu wa nyumba za
waganga,ukosefu wa dawa zikiwemo za kuvubaza makali ya virusi vya
UKIMWI na kwamba kwa sasa wanasafiri umbali wa zaidi ya kilomita 50
kwenda kupata tiba hiyo kutokana na zahanati hiyo kuwa haina uwezo
wa kutoa huduma hiyo.
Akizungumzia tatizo la kufungwa kwa zahanati hiyo kaimu mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Filbert Mbwiro amesema
kuwa amesikitishwa na kitendo cha kufungwa kwa zahanati hiyo na
kwamba ni kinyume cha sheria kwa watumishi wa afya kufunga zahanati
na kuondoka wote kuelekea kwenye semina na kwamba atalifuatilia
halmashauri kujua aliyetoa barua ya kwenda kwenye semina kwa
watumishi na kufunga zahanati hiyo.
Aidha bwana Mbwiro amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa
watumishi hao mara tu itakapobainika wameondoka pasipo utaratibu
nakuwataka radhi wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki wakati
taratibu za kuwatafuta wauguzi hao ili kuendelea kutoa huduma
zikiendelea katika zahanati hiyo.
Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini bwana Deo Sanga amemuagiza
kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kuhakikisha
zahanati hiyo inafunguliwa mapema iwezekanavyo na kwamba watumishi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment