Mwanafunzi mmoja wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 13 katika shule ya msingi Matembwe Filbert Luwanja jana amezama kwenye bwawa la maji lililopo katika kijiji hicho wakati akiogelea na wenzake ambapo mtoto huyo hajaweza kupatikana mpaka leo.
Akizungumza Na Uplands fm mwenyekiti wa kitongoji wa Itundu bwana Justin Mfugale amesema kuwa taarifa za kuzama kwa mtoto huyo tayari zimefikishwa katika kituo cha polisi Lupembe na kwamba jitihada mbalimbali zinaendelea za kumtafuta mtoto huyo.
Daniel Nyarusi ni Mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpaka sasa wataalamu mbalimbali wa kuogelea wanaendelea kumtafuta mtoto huyo kwenye bwawa la maji hilo.
Aidha bwana Nyarusi amesema kutokana na jitihada za kuogelea kutozaa matunda tangu jana walipoanza kuogelea kutafuta mtoto huyo aliyezama kwenye maji hayo ameiomba halmashauri ya wilaya ya Njombe kuwasaidia wataalamu ambao wanauwezo wa kuzama ndani ya maji ili kumtafuta mtoto huyo anadaiwa kuzama ndani ya maji hyao.
Sambamba na hayo zaidi ya Ekali elfu moja za mashamba ya miti za wananchi,taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali zimeteketea kwa moto tukio lililotokea jana majira ya saa sita,na saa saba za mchana katika kijiji hicho.
Akizungumza na Uplands fm mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe bwana Daniel Nyarusi amesema chanzo cha tukio hilo hakijafahamika ambapo amesema kuwa inasemekana moto huo umetokea katika kijiji cha jirani cha wanginyi kata ya Matembwe.
Aidha bwana Nyarusi amesema kuwa jitihada za kuwabaini waliohusika na uchomaji wa mazingira kwa kuchoma mali mbalimbali katika eneo hilo na kuchukuliwa hatua za kisheria huku akisema anatarajia kwenda kukutana na uongozi wa kijiji cha Wanginyi ili kujua chanzo cha tukio la uchomaji wa moto huo.
Siku chache zilizopita kulitokea tukio la kutumbukia kwa mtu katika bwawa la maji katika kampuni ya Tanwat ambapo mwili wa marehemu ulipatikana baada ya siku sita kutokana na kukosekana kwa wataalamu wa uzamiaji ndani ya maji.
Kuhusu uchomaji mazingira kiholela serikali imekuwa ikisisitiza wananchi kutunza mazingira kwa kutochoma moto mazingira lakini kumekuwa na kukiuka kwa taratibu hizo ambapo mamia ya wakazi wa Njombe wamekuwa wakipoteza mali zao kwa kuchomewa moto miti na mali nyingine za mashambani.
No comments:
Post a Comment