Thursday, July 18, 2013
WANANCHI WA KIJIJI CHA LIMA KATA YA NINGA WILAYANI NJOMBE WAANZA UJENZI WA ZAHANATI BAADA YA KUPATA TABU YA KUKOSA HUDUMA ZA AFYA KWA MUDA MREFU,WAKATI HUOHUO AFISA ELIMU MSINGI AMUTAKA MKUU WA SHULE LIMA KUHAMIA JIRANI NA ENEO LA KAZI MAPEMA KABLA HATUA NYINGINE HAZIJACHUKULIWA.
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI DEO SANGA AKIWA NA WATAALAMU MBALIMBALI WA HALMASHAURI
MBUNGE AKIKAGUA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI KATIKA KIJIJI CHA LIMA KATA YA IKUNA LEO
KAZI HII INAFANYWA NA WANANCHI WOTE AKINA MAMA NA AKINA BABA WOTE WANAJUMUIKA KUFYATUA TOFARI
WANANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI LIMA WAKIWA ENEO LA MKUTANO ULIOFANYIKA KATIKA KIJIJI HICHO
HAPA MBUNGE DEO SANGA MAARUFU KWA JINA LA JA PEOPLE AKIWASILI ENEO LA MKUTANO NA KUPOKELWA NA WANANCHI VIZURI
KATIBU MWENEZI CCM MKOA WA NJOMBE HONORATUS MGAYA AMESEMA CHAMA SIYO KIBAYA ILA WATU NA VIONGOZI WALIOKO NDANI YA CHAMA HICHO NDIYO WABAYA
DIWANI KATA YA NINGA AKIMKARIBISHA MBUNGE KUONGEA NA WANANCHI
MBUNGE NA WATAALAMU MBALIMBALI WA HARIMASHAURI WAKIWASILI KATIKA KIJIJI CHA ISITU
NI WANANCHI WA KIJIJI CHA ISITU HAPA KATA YA NINGA WAKIMPOKEA MGENI RASMI
AFISA TAARAFA WA LUPEMBE
HAPA NI KIJIJI CHA ISITU AMBAPO NI MKUTANO WA MWISHO KWA SIKU YA LEO
JAMANI TUWALEE WATOTO VIZURI TUWAPE HAKI ZAO ZA MSINGI IKIWEMO CHAKULA,MALAZI NA ELIMU NI HAKI YAKE,VIATU TUWAVISHE HATA KAMA TUNA HALI NGUMU HAWA NI WATOTO WAZURI WAKIWA KWENYE MKUTANO WA MBUNGE DEO SANGA KATIKA KIJIJI CHA ISITU.
Kaimu afisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Emmanuel Mayemba amemutaka mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lima na walimu wengine kuhamia jirani na vituo vya kazi kwani hakuna sababu ya msingi ya walimu hao kuishi mbali na mahala pa kazi.
Agizo hilo la kaimu afisa elimu huyo bwana Mayemba limefuatia malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho ya kwamba mkuu wa shule hiyo haishi jirani na shule licha ya wananchi kujengta nyumba za walimu hali inayorudisha nyuma taaruma kwa wanafunzi.
Wakizungumza mara baada ya mkutano huo kuahirishwa baadhi ya walimu na watumishi wengine wa serikali katika kijiji hicho wamekili kuwepo kwa tatizo hilo lakini ni siku za wikendi ambapo watumishi wengi huwa wanakwenda katika kijiji cha Ninga kutokana na kukosekana kwa huduma za matibabu na kusema kuwa msimu wa masika miundombinu huwa haipitiki.
Katika taarifa fupi ya kijiji iliyosomwa na mwalimu wa shule ya msingi Lima kwa niaba ya afisa mtendaji wa kijiji hicho imeelezea ujenzi wa zahanati ambao kwa sasa unaendelea kijijini hapo ambapo ili kuunga mkono ujenzi huo halmashauri ya wilaya ya Njombe imechangia milioni 35 huku wananchi wakichangia kufyatua tofali na shughuli nyingine za ujenzi.
Mbunge wa jimbo hilo bwana Deo Sanga amesema lengo la kutembelea kijiji hicho ni kutaka kukagua miradi inayotekelezwa na wananchi ambapo pamoja na mamo mengine ameagiza serikali ya kijiji hicho kuhakikisha wajane wote wanaandikishwa na kuingia kwenye mgao wa pembejeo hizo.
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya amepongeza kwa jitihada zinazofanywa na wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao na kuwataka viongozi wa vijiji,vitongoji na kata kuhakikisha wanakusanya michango ya miradi inayotekelezwa vijijini mwao kwa umakini ili kuepukana na migogoro isiyo ya lazima......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment