Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, July 18, 2013

MBUNGE WA NJOMBE KASKAZINI ATOA VIFAA VYA MICHEZO KILA KIJIJI NA KATA KATIKA JIMBO LAKE

Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini amesema ili kuinua vipaji kwa vijana ni vema wadau wa michezo wakatambua umuhimu wa michezo kwa kuhamasisha michezo kwa vijana kuanzia watoto wa shule za msingi hadi sekondari kwa kuwapa uzoefu katika michezo mbalimbali.

Akizungumza na wananchi akiwa katika ziara ya kutembelea kata mbalimbali za jimbo lake Mbunge wa jimbo hilo bwana Deo Sanga amesema kwa sasa amejipanga kikamilifu kuhakikisha anawafikia wananchi wote kwa kuhamasisha miradi ya maendeleo na michezo ambapo kila kata na vijiji anavyopita kufanya mikutano anakabidhi vifaa vya michezo kwa vijana.

Vifaa ambavyo bwana Sanga anakabidhi ni pamoja na mpira wa miguu kwa wavulana pamoja na jez seti moja kwa kila kijiji ambacho kimeunda timu ya mchezo wa mpira wa miguu ambapo amesema lengo kubwa ni kuwataka wananchi kujikita zaidi katika shughuli za kijasiliamali na baada ya kazi waende katika viwanja vya michezo kushiliki michezo ya mpira.

Ili kupunguza uharifu katika vijiji na mitaa amesema vijana wanatakiwa kuacha tabia ya kushinda vijiweni badala yake wafanye kazi ili kujikwamua kiuchumi kwa maslahi yao na ya baadae huku akisema ni vema wakaepukana na matumizi ya madawa ya kulevya na kujenga afya zilizo bora.

No comments:

Post a Comment