Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii
kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na
ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji kutoka Walter Reed
Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20
iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini
Mbeya.
Mkufunzi huyo amesema kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji
wa Kijinsia ndani ya jamii vinaweza kumalizwa endapo Wanahabari watafanya kazi
ya kujitolea ya kuibua na kuiambia jamii madhara ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya jamii ya Mbeya
inasadikika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwamba Mfuko wa
raisi wa Marekani umetoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha Vitendo hivyo vinaisha
ambapo msaada huo utalenga Nchi tatu ikiwemo Tanzania.
Amesema Nchini Tanzania ni Mikoa minne itakayohusika
ambayo ni Mbeya, Iringa, Mara na Dar Es Salaam ambapo kwa Mkoa wa Mbeya
ni Wilaya Sita zitakazohusika ambazo ni Mbeya Jiji, Ileje, Kyela, Rungwe,
Busokelo na Mbeya Vijijini.
|
No comments:
Post a Comment