Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, June 8, 2013

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKEMEA VITENDO VYA UNYANYASAJI KWA AKIMAMA,AWATAKA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA WANAOHUSIKA NA VITENDO HIVYO.

 MKUU WA WILAYA YA MAKETE JOSEPHINA MATIRO AKIONGOZA KONGAMANO KAMA MC.
 MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA IRINGA LEDIANA MNG'ONG'O AKIZUNGUMZA NA WANAKONGAMANO.

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIWAKARIBISHA WAGENI VALENCE KABELEGE

 MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA IRINGA LEDIANA MNG'ONG'O






 MWAKILISHI WA UBAROZI WA MAREKANI UKANDA WA KUSINI 


 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE AZUNGUMZE NA AKINA MAMA HAO.

 AKITOA HOTUBA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE.

 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA LUSINGA  KATA YA LUPALILO WILAYANI MAKETE AKITOA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI AKINA MAMA NA WATOTO KATIKA ENEO ANALOONGOZA.




 WAANDISHI WA HABARI WAKIMUHOJI MKUU WA WILAYA YA MAKETE JOSEFINA MATIRO KUHUSIANA NA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI  KATIKA WILAYA YAKE.


 PICHA YA PAMOJA YA WANAWAKE WAKIWA NA MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI
 MIONGONI MWA VIONGOZI WA AKINA MAMA AKIELEZEA JINSI WANAWAKE WANAVYOFANYIWA VITENDO VYA UKATILI KATIKA MAENEO YAO.
MKURUGENZI WA KITUO CHA KUTOA MSAADA KWA WATOTO NA AKINA MAMA WALIOFANYIWA VITENDO VYA UKATILI  MKOA WA IRINGA BI ESTER SANGA AKIWA AKIWASILISHA  MADA KATIKA KONGAMANO LILILOFANYIKA UKUMBI WA HALMASHAURI  YA WILAYA YA NJOMBE.Kwa ushirikiano wa wadau wa mtandao huu Prosper Mfugale na Sunday Bavugha.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kaptein Mstaafu Asery Msangi  Leo Amezindua Rasmi Kongamano la Wanawake na Viongozi Wanawakea Mkoa wa Njombe na Kuwataka Wanawake na Wasichana Waliofanyiwa Vitendo Vya Unyanyasaji wa Kijinsia na Ukatili Kutoa Taarifa Kwenye Vyombo Vya Sheria Ili Watu Wanaojihusisha na Vitendo Hivyo Wachukuliwe Hatua za Kisheria.

Aidha Kaptein Mstaafu Msangi Amewataka Wanawake Kushirikiana na Serikali Katika Kupambana na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Kwa Kuwakataa Wanaume Ambao Hawajafanyiwa Tohara Kwani Itasaidia Kuhepukana na Maambukizi ya Magonjwa Mbalimbali Ikiwemo Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Halikadhalika Mkuu Huyo wa Mkoa Amewaomba Wanawake Kujitokeza Kwa Wingi Kutoa Maoni ya Rasimu ya  Katiba Mpya Ili Masuala ya Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia Yaweze Kuzingatiwa

Katika Hatua Nyingine Kapteni Mstaafu Msangi Ameelezea Mpango Mkakati wa Kupambana na Maambukizi ya Ukimwi Kwa Miaka Mitatu Ikiwemo Kampeni ya Tohara Kwa Wanaume.

Kwa Upande Wao Baadhi ya Washiriki wa Kongamano Hilo Wameelezea Hali ya Ukatilii na Unyanyasaji  na Kusema Kuwa Kwa Sasa Imepungua Tofauti na Ilivyokuwa Hapo Awali.

No comments:

Post a Comment