Wednesday, June 19, 2013
WAKAZI SABA WA KATA YA KIPENGELE WAMEFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE KUJIBU TUHUMA ZINAZOWAKABILI ZA MAKOSA MATATU
HILI NI DIRISHA LA KIBANDA CHA BIASHARA CHA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA KIPENGELE KILICHOCHOMWA MOTO NA BAADHI YA WATU WANAOSHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
BOMA LA NG'OME LA MZEE MMOJA WA KIJIJINI HAPO AMBALO NI MIONGONI MWA YALIOCHOIMWA NA WATU SABA WANAODADIKIKA NDIYO WALIOHUSIKA NA UCHOMWAJI WA MALI HIZO IKIWEMO BENDELA YA SERIKALI YA KIJIJI KWA KILE KILICHODAIWA NI KUWA SERIKALI ILIAMURU KUKATWA MITI MICHACHE YA WANANCHI ILIOKO KWENYE MARISHO YA VIONGOZI IKAACHWA.
Wakazi Saba wa Kijiji cha Kipengele Wilaya ya Wanging'ombe Ambao ni Ndugu Wamefikishwa Kwa Mara ya Kwanza Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe Wakikabiliwa na Makosa Matatu Likiwemo la Kuchoma Moto Ofisi ya Kata
Akisoma Hati ya Mashtaka Mbele ya Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo , Mwendesha Mashtaka Selapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Washtakiwa Walitenda Kosa Hilo Juni 11 Mwaka Huu Kijijini Humo.
Imedaiwa Mahakamani Hapo na Mwendesha Mashtaka Kuwa Washtakiwa Wanakabiliwa na Makosa Mengine Mawili ya Kuchoma Moto Duka na Boma la Ng'ombe Pamoja na Bendera ya Ofisi ya Kata Hiyo.
Mwendesha Mashtaka Matiku Amewataja Washtakiwa Hao Waliofikishwa Katika Mahakama Hiyo Kuwa ni John Chengula, Gaspari Chengula, Nicolaus Chengula,Yustini Sanga,Yubert Chengula na Godwin chengula
Hata Hivyo Washtakiwa Walipohojiwa Kutenda Kosa Hilo Wamekana Mbele ya Mahakama , Huku Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Akiarisha Kesi Hiyo Hadi Julai Tatu Mwaka Huu Upelelezi Utakapokamilika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment