Monday, June 17, 2013
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE AMEKEMEA WAZAZI KUWANYANYASA WATOTO,AAGIZA WATENDAJI WA WILAYA HIYO KUFUATILIA SUALA HILO..
WANAFUNZI MBALIMBALI WA KATA YA IGIMA WAKIONESHA BURUDANI MBALIMBALI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
WAGENI MBALIMBALI AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE WAKIWASILI KATIKA UWANJA WA SHEREHE
TAMADUNI MBALIMBALI ZA MICHEZO ZIKIONESHWA MBELE YA MGENI RASMI
NI HARAMBEE KWAAJILI YA MTOTO YATIMA ALIYEONESHA KIPAJI CHA KUIMBA MBELE YA MGENI RASMI HUKU MAVAZI YAKE YAKIWA YAMECHAKAA NA AFISA TAARAFA WA WANGING'OMBE AKAAMU KUITISHA HARAMBEE
KATIBU TAWALA WA WILAYA YA WANGING'OMBE AKIJITAMBULISHA
AFISA USTAWI WA JAMII AVERINO CHAULA AKISOMA TAARIFA YA SIKU YA MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA JANA
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ESTERINA KILASI AKITOA HOTUBA KWA WANANCHI NA WATOTO MBALIMBALI AKIWA KATA YA IGIMA YALIKOFANYIKIA MAADHIMISHO HAYO
DIWANI WA KATA YA IGIMA NA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE LUKERO NYAGAWA AKIWAMBIA WANANCHI KWAMBA ATAHAKIKISHA ANAMSOMESHA HADI KIDATO CHA SITA NA KUMPATIA MAHITAJI YOTE
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi. Esterina Kilasi Amewataka Wananchi Wilayani Humo Kuachana na Mila na Desturi Potofu Zinazowakandamiza Watoto Pamoja na Kukomesha Vitendo Vya Unyanyasaji na Ukatili Kwa Watoto.
Akizungumza Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Yaliofanyika Jana Wilayani Humo Mkuu Huyo wa Wilaya Amesema Hadi Kufikia Sasa Jumla ya Watoto 85 Wamebakwa Wilayani Humo,Jambo Linaloashiria Ukubwa wa Tatizo la Ukatili Kwa Watoto Wilayani Humo.
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Amekemea Tabia ya Baadhi ya Wazazi Wenye Tabia ya Kuwaficha Watoto Wenye Ulemavu na Hivyo Amewaagiza Watendaji wa Vijiji na Kata Kufuatilia Suala Hilo.
Awali Akisoma Taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Katika Maadhimisho Hayo , Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Njombe Averino Chaula Amesema Matukio ya Unyanyasaji na Ukatili Yamekuwa Yakiongezeka Kwa Kasi Wilayani Humo Kutokana na Sababu Mbalimbali Ikiwemo Uelewa Mdogo wa Jamii Kuhusu Haki za Watoto
Katika Taarifa Hiyo Halmashauri Inatarajia Kuongeza Jitihada za Kupambana Dhidi ya Vitendo Hivyo Kwa Kuwakamata na Kuwachukulia Hatua za Kisheria Watu Wote Wanaojihusisha na Vitendo Hivyo.
Kwa Upande Wake Diwani wa Kata ya Igima Ambaye Pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Lukero Nyagawa Ameahidi Kumsomesha na Kumpatia Mahitaji Yote ya Shule Mtoto Menrick Luvanza Ambaye ni Yatima na Mwanafunzi wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Mawindi Hadi Kidato cha Sita
Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Huandaa na Kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika Kila Mwaka Juni 16 Kama Nchi Nyingine Duniani Ambapo Kauli Mbiu ya Maadhimisho Hayo Kwa Mwaka Huu ni KUONDOA MILA ZENYE KULETA MADHARA KWA WATOTO,NI JUKUMU LETU SOTE .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment