Tuesday, June 18, 2013
DIWANI KATA YA KIPENGELE AAHIDI KUONDOA MITI YOTE PASIPO KUJALI YA KIONGOZI WA SERIKALI MITI NILIYOPANDWA KATIKA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI NYA MARISHO.
HILI NI DIRISHA LA KIBANDA CHA BIASHARA CHA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA KIPENGELE KILICHOCHOMWA MOTO NA BAADHI YA WATU WANAOSHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
BOMA LA NG'OME LA MZEE MMOJA WA KIJIJINI HAPO AMBALO NI MIONGONI MWA YALIOCHOIMWA NA WATU SABA WANAODADIKIKA NDIYO WALIOHUSIKA NA UCHOMWAJI WA MALI HIZO IKIWEMO BENDELA YA SERIKALI YA KIJIJI KWA KILE KILICHODAIWA NI KUWA SERIKALI ILIAMURU KUKATWA MITI MICHACHE YA WANANCHI ILIOKO KWENYE MARISHO YA VIONGOZI IKAACHWA.
Diwani wa Kata ya Kipengele Bwana Lukemelo Mgaya Ameagiza Kukatwa Kwa Miti Yote Iliyopandwa Kinyume cha Sheria Kwenye Eneo Lililokuwa Limetengwa Kisheria na Serikali ya Kijiji cha Kipengele Kwa Ajili ya Malisho ya Mifugo Pasipo Kujali Mliki wa Miti Hiyo Kuwa ni Kiongozi wa Serikali .
Diwani Mgaya Ametoa Agizo Hilo Kwenye Mkutano wa Hadhara Kufuatia Malalamiko Yaliyotolewa na Baadhi ya Wananchi wa Kijiji Hicho Kuwa Kuna Baadhi ya Miti Haijakatwa Katika Eneo Hilo Inayosadikiwa Kuwa ya Viongozi .
Akizungumza na Kituo Hiki Mara Baada ya Kumalizika Kwa Mkutano Diwani Mgaya Amekiri Kuwepo Kwa Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Kijiji Wanaomiliki Miti Katika Eneo Hilo la Malisho na Kuesema Kuwa Mara Baada ya Taratibu Zote za Kisheria Kukamilika na Miti Iliyopandwa Ndani ya Eneo la Malisho Itaondolewa.
Awali Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Wananchi Hao Wamelalamikia
Kitendo cha Uongozi wa Kijiji Kuruhusu Kukatwa Miti ya Wananchi Pekee Yao Huku Miti ya Viongozi Ikiachwa Suaal Ambalo Wamesema ni Uonevu Kwa Wananchi wa Kawaida
Haward Mwanganya ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipengele Ambaye Amekanusha Tuhuma Zilizoelekezwa Kwa Uongozi wa Kijiji na Kusema Kuwa Hakuna Kiongozi wa Serikali ya Kijiji Hicho Aliyehusika na Upandaji Miti Ndani ya Eneo Hilo.
Bwana Mwanganya licha ya kukanusha madai ya wananchi wa kijiji hao lakini amekiri kuwepo kwa miti ambayo amedai ni ya mkewe aliye zaa nae na si viongozi wa kijiji kuhusika kupanda miti katika eneo hilo.
Wiki Iliyopita Wakazi Saba wa Kijiji cha Kipengele Walishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kwa Tuhuma za Kuchoma Ofisi ya Kata , Kibanda cha Biashara cha Mwenyeki wa Kijiji Hicho , Boma la Mifugo la Mkazi wa Kijiji Pamoja na Bendera ya serikali Kwa Kile Kinachodaiwa ni Kulipiza Kisasa Baada ya Uongozi wa Kata ya Kipengele Kutoa Amri ya Kukatwa Kwa Miti Iliyopandwa Ndani ya Eneo Lililotengwa Kwa Ajili ya Malisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment