CHANZO CHA HABARI HII NI FRANCIS GODWIN BLOG
BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu.
Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha Kalole, Tarafa ya Kisiju, wilayani humo.
Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari
Salum, mwaka 2010 ndugu wa mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi
Charambe Mbagala, jijini Dar alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe
mtoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’.
Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa
muda mfupi aliugua malaria, baba mtu akapewa taarifa na kufika Dar kwa
ajili ya kumuona mwanaye aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar.
Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili
na kufanikiwa kuzungumza machache na mwanaye huyo ambapo alikuwa
akilalamikia maumivu ya tumbo.
Mzee huyo alisema ilibidi aondoke licha
ya mwanaye kumtaka alale lakini kwa vile yeye ni mwanaume
isingewezekana kulala hospitalini hapo.
“Kesho yake nilipewa taarifa kuwa
mwanangu amefariki dunia usiku. Tulianza taratibu za mazishi na kumzika
kwenye Makaburi ya Kichangani, Mbagala, Dar kutokana na kukosa fedha za
kuusafirisha mwili hadi Mkuranga,” alisema mzazi huyo
Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa
jina la Said Ali Ngaora ‘Dr. Lamba’ anayeishi Mbagala Rangi Tatu, Dar
alifika katika kijiji hicho cha Kalole mwaka huu na kuwaambia wananchi
kuwa kijijini hapo pana mtu anaonekana alikufa na kuzikwa lakini bado
yupo hai na amewekwa sehemu na kutaja gharama za kumtoa ni shilingi
milioni tatu.
Akielezea tukio zima Dr. Lamba alisema wananchi walimruhusu akaanza kazi kwa kushirikiana na wataalamu wenzake.
Dr. Lamba na timu yake walifanikiwa
kumuibua msichana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 12-15 kwenye mji
ambao hakuna mtu anayeishi akiwa ndani ya banda la kuku huku kukiwa na
chungu chenye damu, asali na udongo ambavyo vilikuwa ndivyo vyakula
vyake akiwa na muonekano wa kutisha kwa kuwa na nywele ndefu na chafu na
kucha zikiwa ndefu mithili ya jini.
Baada ya kumtoa alipelekwa katika
uwanja wa mpira kijijini hapo na kuogeshwa pamoja na kukatwa kucha kisha
akapelekwa katika nyumba aliyofikia mganga huyo, hata hivyo hakuweza
kuongea vizuri.
Kwa mujibu wa mashuhuda ulimi wa Nuru
ulikuwa mzito na mpaka sasa anazungumza kwa vitendo kama bubu huku
chakula ambacho ameanza kula vikiwa ni ugali na kuku, uji na juisi ya
embe.
Mbali na shilingi milioni tatu za
kutoa, mganga huyo anataka milioni 15 kutokana na dawa anazompa kwa
ajili ya matibabu ili arudi katika hali ya kibinadamu .
Hata hivyo, baadhi ya ndugu wanaopinga
kuwa Nuru siyo mtoto wao lakini baba mzazi anasema ni mwanaye kutokana
na alama zilizopo mgongoni mwake na anafanana sana na mdogo wake.
No comments:
Post a Comment