OFISI YA KIPENGELE SACCOS WILAYANI WANGING'OMBE ILIYOPO KIJIJI CHA KIPENGELE.
Mhuhasibu wa SACCOS ya Kipengele wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe George Mbwiro.
Chama Cha Akiba na Mikopo, Kipengele SACCOS Kimewataka Wanachama wa Chama Hicho,Hasa Wale Walionufaika na Mikopo Inayotolewa na Chama Hicho Kuitumia Vizuri Mikopo Hiyo Kwa Kujiinua Kiuchumi na Kuongeza Kipato Ili Kuondokana na Hali ya Umaskini.
Aidha Chama Hicho Kimewasisitizia Wanachama Hao Kuhakikisha Wanarejesha Mikopo Hiyo Kwa Wakati Ili Kuwezesha Wanachama Wengine Kuweza Kunufaika na Mikopo Hiyo.
Akizungumza na mtandao huu Meneja wa Kipengele SACCOS Bw Frank Saboso Amesema Mikopo Inayotolewa na Chama Hicho Imelenga Kuwainua Kiuchumi Wanachama Hao Katika Masuala ya Kilimo na Biashara na Kusema Hayo Yamekuwa ni Sehemu ya Malengo ya Chama Hicho Tangu Kilipoanzishwa Mwaka 2010.
Amesema Pamoja na Kutoa Mikopo Hiyo Pia Chama Hicho Kimekuwa Kikitoa Elimu Kupitia Mikutano ya Hadhara,Elimu Ambayo Imelenga Kuwawezesha Wananchi Kuweza Kujiinua Kiuchumu.
Akielezea Baadhi ya Changamoto Zinazokikabili Chama Hicho Mhasibu wa Chama Hicho Bw Geoge Mbwiro Amesema ni Pamoja na Baadhi ya Wanachama Kutotoa Taarifa Sahihi Pindi Wanapohitaji Mikopo Jambo Ambalo Limekuwa Likisababisha Usumbufu Mara Kadhaa.
Chama cha SACCOS Kipengele kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na wanachama sabini ambapo kwa sasa kinawanachama zaidi ya mia mbili ambao ni hai.
No comments:
Post a Comment