CHANZO Mahmoud Ahmad,Arusha
Jeshi
la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo
(CHADEMA) kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye
viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye
viwanja hivyo huku mabomu yakirindima uwanjani hapo.
Akizungumza
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu
upelelezi.
Kamanda Sabas alisema kuwa kwa hiyo jeshi hilo limewataka viongozi wa
chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia
shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali
kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangia juzi kwa wafuasi
wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya
kuomboleza tukio la bomu la kurushwa kwa mkono lililotokea uwanjani hapo
juzi.
Hata
hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikuwa
wamukusanyana kwenye uwanja huo hali iliyoendelea kuleta mvutano kati ya
viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya
jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.
Baadhi
ya viongozi wa juu wa chama hicho walikuwepo uwanjani hapo akiwemo
mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje na wabunge mbali
mbali wa chama hicho walikuwa kwenye kikao cha bunge kinachoendelea hali
hiyo imeliweka jiji hili kusimama shughuli zake kutokana na mabomu
hayo.
No comments:
Post a Comment