Na Mbeya yetu Blog
Daladala ambayo ilikuwa inatoka Mbalizi kwenda Songwe yenye namba za
usajili T 635 ALS ikiwa imeharibika vibaya Baada ya Ajali kutokea Eneo
la Ifisi Mbalizi Mbeya
Hapa
ndipo eneo ambalo Daladala iliingia wakati ilijaribu kulipita Gari
lengine akiwa mwendo kasi na kuukutana na Tela la Mafuta
Daladala upande wa nyuma
Lori aina ya Scania yenye namba ZA usajili T378 AGD likiwa limepaki Baada ya ajali hiyo kutokea
Mabaki ya daladala
Wananchi mbalimbali wakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliyo tokea Ifisi Mbalizi Mbeya
Hivi ndivyo Daladala inavyo onekana upande wa Mbele baada ya Ajali kutokea
Dereva wa daladala ambaye ndiye aliye sababisha ajali hiyo Nikutusya Mwanja akiwa anapelekwa chumba cha matibabu ya Haraka.
Baadhi ya Majeruhi waliokuwemo katika ajali hiyo
Wakazi mbalimbali wakiwa katika Hospitali ya Ifisi Mbalizi Mbeya kutazama ndugu zao waliopata ajali.
Askari wa usalama barabarani wakiandikishana Dhamana na ndugu wa Dereva wa Daladala ili apate dhamana ya kutibiwa
*****************
WATU 17 wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kuharibika vibaya kufuatia ajali iliyohusisha Gari la abiria aina
ya Toyota Hiace na Scania.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya Saa Saba Mchana katika eneo la
Ifisi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Ifisi(ICC) Mbeya Vijijini.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema gari la abiria Toyota
Hiace lenye namba za usajili T 635 ALS likiendeshwa na Nikutusya Mwanja
likitokea Mbalizi kuelekea Songwe iliingia kwenye Trela la Scania lililokuwa
likitokea Tunduma kuelekea Dar Es Salaam.
Wamesema chanzo cha ajali hiyo
ni mwendokasi wa gari ndogo ambapo Dereva alikuwa akijaribu kulipita gari lingine
lakini mbele akakutana na Lori ambalo alipojaribu kulikwepa akaingia kwenye
Trela lake na kupinduka vibaya.
Trela hilo lenye namba za
usajili T 675 ACT likiwa linavutwa na Kichwa chenye namba za usajili T 378 AGD
halikuweza kuumia sana kutokana na kwenda kwa mwendo mdogo ambapo majeruhi wote
wamekimbizwa katika Hospitale teule ya Ifisi kwa matibabu zaidi.
Muuguzi Msaidizi wa Hospitali
Teule ya Ifisi Elimath Sanga amethibitisha kupokelewa kwa majeruhi 17 na kwamba
kati ya majeruhi hao 3 hali zao siyo nzuri sana ingawa majina yao hayakuweza
kupatikana.
Ameongeza kuwa majeruhi wengi
wameumia sehemu za kichwani na miguuni na kwamba baada ya kumaliza kupatiwa
huduma ya kwanza wataangalia ni wangapi wanaweza kuruhusiwa na wengine kulazwa.
Hata hivyo habari kutoka eneo la
tukio zimesema kuwa Kondakta wa gari dogo aliyefahamika kwa jina moja la Ayubu
alitoweka mara baada ya kutokea kwa ajali ingawa haifahamiki kama ni kurukwa
kwa akili au ni kukimbia kesi.
No comments:
Post a Comment