MAUAJI
ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara
baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja
kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha
na vitendo vya kishirikina.
Pia
watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba
walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza
nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa
wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa
mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa,
tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira
kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua
kijana huyo hivi karibuni.
Kwa hisani ya Mpekuzi blog
Kijana huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga
alidai hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa tangu
azikwe kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za
usiku pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo
wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo.
Wakiwa kwa mganga,wanafamilia hao walitajiwa majina ya wanakijiji watatu wa kijiji hicho ambao
hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja na familia zao
kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na kuangushiwa adhabu hizo
za kinyama.
Wa
kwanza kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye
alikimbilia kijiji cha jiorani kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya, ambapo
walimkata miguu yote miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla
ya kumchoma moto ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua
nguo zake tu huku mwili ukiwa upo vile vile.
Baadaye
walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama
kama rafikie kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa
kuamini huenda wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye
kurudi Kasaula na kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia
ajuza hao wengine kisha kuchoma nyumba tatu.
Bibi
wa tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo,
lakini nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga
kuporwa na watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo
kuwachoma na kuwala kwa hasira.
Kamanda
wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo
la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka
waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.
No comments:
Post a Comment