Monday, May 27, 2013
MAMA MJAMZITO MKAZI WA KATA YA MTWANGO APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA MKOANI NJOMBE
HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA ITUNDUMA WAKIWA NA VIONGOZI WAO WAMEKUSANYIKA NJE KIDOGO NA HOSPITALI YA KIBENA WAKIJADILI KWA KUMTAFUTIA MAMA ALIYE POTEA
HUYU MAMA NDIYE ALIYEPOPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA KATIKAM HOSPITALI YA KIBENA NJOMBE NA ALIYESHIKA DAFTARI NI SHEMEJI YAKE PICHA HII WALIPIGA WAKIWA NYUMBANI KWAO KABLA HAJAPATA UJAUZITO NA KABLA HAJATOWEKA KWENYE MAZINGIRA HAYO
HII NI HOSPITALI YA KIBENA
Mama Mmoja Mjamzito Mkazi wa Kijiji Cha Itunduma Wilayani Njombe
Jestina Zabron Mhema Miaka 23 Amepotea Katika Mazingira ya
Kutatanisha,Akiwa Katika Hospitali ya Kibena Mjini Njombe Wakati
Akisubiri Kujifungua.
Aidha Kutokana na Tukio Hilo Wananchi wa Kijiji Hicho Wameiomba
Serikali Kuimarisha Ulinzi Hospitalini Hapo Ili Kuzuia Matukio Kama
Hayo Yasiweze Kujitokeza Kwa Mara Nyingine Tena Katika Hospitali
Hiyo.
Wakizungumza na Uplands Fm Kwa Masikitiko Makubwa Hospitalini Hapo
Wananchi wa Kijiji Hicho,Pamoja na Kushangazwa na Tukio Hilo Pia
Wameelezea Masikitiko Yao Juu ya Tukio Hilo na Kusema Uongozi wa
Hospitali Unapaswa Kuwa Makini Katika Ulinzi na Namna ya Kuwalinda
Wagonjwa.
Yustin Nyagawa ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Itunduma na Pasval
Kaduma ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibena Hospitali Wanawaomba
Wananchi Kushirikiana Ili Kuweza Kumtafuta Mama Huyo Kwa Kuwa
Taarifa za Awali Zinaonesha Kuwa Hakuna na Matatizo ya Akili Hivyo
Huenda Amepotea Katika Maeneo ya Jirani na Hospitali Hiyo.
Imedaiwa Kuwa Mama Huyo Alipotea May 26 Mwaka Huu Majira ya Saa
sita Mchana Baada ya Kukaa Hospitalini Kwa Zaidi ya Wiki Moja Sasa
Akisubiri Kujifungua.
Hata hivyo jitihada za wananchi za kumtafuta mama huyo hazikuwa ma matunda yoyote ambapo wameahirisha kwa leo wataendelea tena na zoezi la kumtafuta mama huyo hapo kesho wakiwa wameongozana na wananchi wote wa kijiji hicho na vijiji vya jirani.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe kamishna msaidizi wa polisi Fulgence Ngonyani amekili kupokea taarifa za kupotea kwa mama huyo katika hospitali ya kibena na kusema kuwa jitihada za jeshi hilo bado zinaendelea huku akiwataka wananchi mkoani hapa kutoa taarifa mapema pindu wamuonapo mahala popote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment