Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, May 1, 2013

MHANDISI MSAIDIZI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AFARIKI DUNIA KWA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe acp Fulgency Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo.
 Mhandisi Msaidizi wa maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe enzi za Uhai Wake akisoma taarifa ya hali ya maji katika Mji wa Njombe wakati wa kilele cha Wiki ya Maji machi 22 mwaka huu katika tarafa ya Igominyi Njombe.
 Waokoaji wa kikosi cha Zima moto na baadhi ya wananchi  wakitoa mwili wa Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah Hassan Mgambo.

Mkazi Mmoja wa Mtaa wa Joshoni Mjini Njombe Abdalah Hassan Mgambo

Ambae Pia ni Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Mji wa Njombe Amefariki Dunia

Baada ya Kutumbukia Kwenye Kisima Cha maji Eneo la Turbo Mjini Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha

Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kusema Kuwa Mwili wa Marehemu Uliopolewa Leo.

Majira ya Saa Nane Mchana na

Kusema Kuwa Huenda Mtu Huyo Alijitumbukiza

Kwenye Kisima Hicho Tangu Jana Usiku .

Amesema Chanzo Cha Tukio Hilo Huenda ni Msongo wa Mawazo Aliokuwa Nao

Marehemu Kwa Kuwa Nyaraka Zote Muhimu za Marehemu Zilikutwa Nje ya
Kisima na Hakuna Mtu Anaeshikiliwa Hadi Sasa Huku Uchunguzi Ukiendelea.

Wakati Huo Huo Watu Watatu Wamefariki Dunia Mkoani Njombe Katika Ajali ya

Barabarani Iliotokea Jana Barabara ya Lusisi-Mdandu Wilayani Wanging'ombe.

Akizungumza Kwa Niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency

Ngonyani,Mrakibu Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Njombe Focus Malengo Amesema

Katika Ajali Hiyo Ilihusisha Gari Aina ya Pick Up Yenye Namba za Usajili T 415

AKC Mali ya Kampuni ya Ujenzi ya GS Construchtion ya Iringa Ikiendeshwa na

Boniface Mapunda Mkazi wa Songea ilimgonga Mwendesha Pikipiki Aina ya Sanlg

Yenye Namba za Usajili T 161 BBQ Iliokuwa Ikiendeshwa na Mmoja wa

Marehemu Miongoni Mwa Watu Hao Waliofariki ni Pamoja na Ndugu Wawili wa

Familia Moja Akiwemo Baba na Mtoto Wake.

Amewataja Watu Hao Kuwa ni Daud Fute na Sayuni Fute Wote Wakazi wa Kijiji

cha Mlevela na Bickson Mligo Aliekuwa Dereva wa Pikipiki Iliokuwa Imewabeba

Ndugu Hao

Amesema Chanzo Cha Ajali Hiyo ni Mwendo Kasi Aliokuwa Akiendesha Dereva

wa Gari na Hivyo Jeshi la Polisi Linaendelea Kumtafuta Huku Likitoa Wito Kwa

Madereva Kuzingatia Sheria Pamoja na Kuhepuka Tabia ya Kupakiza Abiria Zaidi

ya Mmoja
 
Aidha Jeshi Hilo Limesisitiza Wananchi Kutekeleza Dhana ya Utii wa Sheria Bila

Shurti Ili Kupunguza Matukio ya Aina Kama Hiyo Mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment