Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, May 22, 2013

MTOTO MWENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA MIWILI AFUNGIWA NDANI ZAIDI YA MIAKA MIWILI NA WAZAZI WAKE IYUNGA JIJINI MBEYA


Mtoto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba  yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha


Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu 

Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana

Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza


Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

Mama wa mlezi wa Joshua akiingia numbani kwake na kutushangaa tumekuja fuatanini kwake

Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo

Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo

Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua

Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema  yeye huwa analala na joshua chumbani kwake 

Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo

Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni



Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo




Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo



Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika  mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
 Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora  pamoja na huduma nyingine.
.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye  Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
 Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
  
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa  wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya  Inyala Kata ya Iyunga  jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo  wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.
Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo


Picha na Mbeya yetu 

No comments:

Post a Comment