WAJASILIAMALI WA CHAMA WA NG'ANDA SACCOS PIA WALIPATIWA ELIMU YA MATUMIZI YA PEMBEJEO ZA KILOMO.
AFISA USHIRIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKITOA MAFUNZO
MWENYEKITI WA SACCOS YA NG'ANDA BI.UPENDO MPINGA
MELKIZEDEK MANDELE AKISOMA RISALA KWA NIABA YA WANACHAMA WOTE WALIOPATIWA MAFUNZO.
DIWANI WA KATA YA IGOSI ELLY CHENGULA AKIONGEA NA WANACHAMA WA NG'ANDA SACCOS
Zaidi ya Wanachama Mia Moja wa Chama Cha Akiba na Mikopo
Ng'anda Wamepatiwa Mafunzo ya Siku Mbili ya Ujasiriamali,Ambapo Pamoja na Mambo
Mengine Wamejifunza Namna ya Utafutaji wa Masoko ya Bidhaa Zao.
Aidha Kutokana na Mafunzo Hayo Wanachama Hao Wametakiwa
Kushiriki Katika Utunzaji wa Mazingira Pamoja na Kutambua Fursa za Kielimu
Zinazoweza Kuboresha Utendaji Wao wa Kazi.
Akizungumza Wakati wa Kufunga Mafunzo Hayo,Diwani wa Kata
ya Igosi Bw Elly Chengula Amesema Mafunzo Hayo ni Muendelezo wa Utekelezaji wa
Mipango ya Viongozi wa CCM Kuwawezesha Wananchi Kujikwamua Kiuchumi.
Ameongeza Kuwa Wanachama wa Vyama Vya Ushirika Wanatakiwa
Kucaha Tabia ya Kuhama Vyama na Badala Yake Wanatakiwa Kukuza Mitaji Yao na
Kuahidi Kushirikiana na Viongozi Wengine Katika Kuviwezesha Vyama Vya Ushirika.
Akisoma Risala Kwa Niaba ya Washiriki wa Mafunzo Hayo
Melkzedek Mandele Pamoja na Kupongeza
Juu ya Mafunzo Hayo,Amesema Bado Wanakabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo
Baadhi ya Wanachama Kutothamini Mafunzo Hayo na Uelewa Mdogo wa Wananchi Kuhusu
Haki na Wajibu Wao.
Miongoni Mwa Mada Zilizofundishwa ni Pamoja na Utafitaji
wa Soko,Elimu ya Msingi ya Bustani za Miti Vijijini,Maana ya Ujasiriamali na
Kilimo Cha Viazi.
Kwa upande wao wanachama waliopatiwa mafunzo ya ujasiliamali katika SACCOS ya Ng'anda wameomba uongozi wa chama hicho kuandaa seimina ya siku saba hadi mwezi ili waweze kunufaika na mafunzo na kuweza kuyafanyia kazi kwani kwa sasa wamepata mafunzo ya muda mfupi.
Wamesema kufuatia kupatiwa mafunzo hayo wanachama hao watakuwa na matarajio mbalimbali ikiwemo kuboresha shughuli za kilimo,biashara,ufugaji pamoja na kufungua bustani za miti na matunda ambapo pia wanatarajia kuunda vikundi vya wakulima,wafugaji, na uoteshaji wa miti ya mbao na matunda
Pamoja na hayo kwa upande wa chama cha Ng'anda Saccos wanatarajia kuwa na wanachama watakaokuwa na matumizi bora ya mikopo,kuboresha miradi yao na kurejesha mikopo kwa wakati pamoja na waliopata mafuinzo kuwa chachu kwa wengine kwa kutoa elimu juu ya kujiunga na SACCOS.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Ng'anda Saccos bi Upendo Mpinga amesema kuna changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanachama kutothamini mafunzo hayo,uelewa mdogo kwa baadhi ya wanachama kuhusu haki na wajibu wao,ushiriki mdogo wa wanachama katika mikutano mikuu ya chama pamoja na chama kukabiliwa na madeni sugu kwa baadhi ya wanachama wasiowaaminifu.
No comments:
Post a Comment