Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, April 24, 2013

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LEO AZINDUA MAADHIMISHO YA CHANJO KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO KIJIJI CHA NYOMBO



 AKIWASIRI KATIKA ENEO LA UZINDUZI WA MAADHIMISHO MKUU WA WILAYA SARAH DUMBA AKIWA MGENI RASMI.
 AFISA TAARAFA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKITAMBULISHA BAADHI YA WAGENI.

 KAIM MGANGA MKUU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE DR CONRAD UGONILE.

 HII NI ZAHANATI YA KIJIJI CHA NYOMBO AMBAPO MAADHIMISHO HAYO YAMEFANYIKA LEO.
 AKITOA HOTUBA KWA WANANCHI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA UZINDUZI WA CHANJO KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO NYOMBO.


 MKUU WA WILAYA ANAFANYA TENDO LA CHANJO KWA BAADHI YA WATOTO WALIOPELEKWA KATIKA ZAHANATI HIYO.


 BAADA YA KUMALIZA TENDO LA CHANJO KWA WATOTO HAO MKUU HUYO ANALREJEO KUCHUKUA SEHEMU YAKE YA KUKAA. picha na Michael Ngilangwa.

Mkuu wa wilaya ya Njombe bi Sarah Dumba leo amezindua chanjo ya watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano katika kijiji cha nyombo ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wazazi na walezi kutambua umuhimu wa kuwapeleka watoto kupatiwa chanjo ili kuwakinga na kuzuia milipuko ya magonjwa.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya   wiki ya chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano  Bi Dumba amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa fursa na kuongeza kasi ya uelewa  kwa jamii juu ya umuhimu wa chanjo katika kuokoa maisha ya watoto wadogo huku akisema malengo ya serikali ni kuifikia jamii isiyotoa kipaumbele katika chanjo ili kuzuia milipuko hiyo.

Aidha bi Dumba ametoa rai kwa wataalamu wanaotoa huduma  za afya kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kupatiwa chanjo wanapata ili kuzuia magonjwa yaliyokusudiwa na kusema kuwa serikali imepeleka chanjo hizo katika vituo vyote vinavyotoa huduma hizo ambapo wananchi wanatakiwa kuunga mkono serikali kupeleka watoto wao .

Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya amewataka viongozi wa vijiji na wananchi kushirikiana na wataalam ili kuwatambua watoto ambao hawajapatiwa chanjo kutokana na Imani potofu na kupatiwa chanjo kufuatana na ratiba iliyotolewa na wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake  kaimu Mganga mkuu  wa halmashauri ya wilaya ya Njombe dr Conrad Ugonile amesema kuwa jamii nyingi huathiliwa na imani potofu juu ya chanjo na kuwaondoa shaka wananchi kwa kusema kuwa chanjo hizo zimetolewa na shirika la afya duniani na kuthibitishwa na Wizara ya afya na Ustawi wa jamii na hazina madhara yoyote kwa atakaye tumia.

Maadhimisho hayo yameanza mnamo mwezi  april 22 na kilele chake kinatarajiwa kufanyika april 29 mwaka huu ambapo ujumbe katika maadhimisho hayo ni JAMII ILIYOPATA CHANJO NI JAMII YENYE AFYA na  kauli mbiu yake ni OKOA  MAISHA  ONDOA ULEMAVU KINGA TAIFA ambapo kiwilaya maadhimisho hayo yamefanyika katika zahanati ya kijiji cha nyombo kata ya Ikuna.

No comments:

Post a Comment