.Katibu mkuu wa Chadema TAIFA Dr.Wilbroad Slaa asema serikali inaacha kuleta maji ya Bomba kwa wananchi inaleta Maji ya washawasha kwa ajili ya kuadhibu wananchi wasiokuwa na hatia.
Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje aking'aka juu ya Misamaha mingi ya kodi inayopoteza mapato ya Taifa.
Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA Wakiwemo Wabunge wa Majimbo mbalimbali kupitia tiketi ya Chadema wakiwa kwenye mkutano Njombe Leo
WENGINE KWENYE MBAO WENGINE KWENYE MAGARI KUSIKILIZA KINACHOTOLEWA NA WABUNGE WA CHADEMA LEO
UMATI WA WANANCHI WALIOHUDHULIA KATIKA ENEO LA UWANJA WA NATIONAL HOUSING MJINI NJOMBE.
JESHI LA POLISI NALO HALIKUCHEZA MBALI KUIMARISHA USALAMA WA RAIA KWENYE MKUTANO HUO MKUBWA WA AJABU KWA UMATI WA WATU MJINI NJOMBE.
VIONGOZI WA CHADEMA WAKIWA JUKWAANI LEO PICHA NA Michael Ngilangwa
.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kimewataka
Wananchi Mkoani Njombe Kuisimamia Serikali na Kuihoji Katika Mambo ya Msingi
Ikiwemo Namna Inavyosimamia Rasilimali za Taifa na Ulinzi wa Raia Pamoja na
Jinsi Serikali Inavyodhibti Matumizi Yake Kwa Ajili ya Kuboresha Maisha ya
Wanancjhi Wake.
Aidha Chama Hicho Pia Kimeitaka Serikali Kuongeza Udhibti
Katika Ukusanyaji wa Kodi Hasa Kwa Wawekezaji Ambao Wamekuwa Wakipata Misamaha
Mingi ya Kodi Jambo Linalochangia Kupunguza Mapato ya Serikali na Hivyo Kuwakosesha
Wananchi Haki yao ya Kunufaika na Rasilimali Zao.
Akizungumza Wakati wa Mkutano wa Chama Hicho Uliofanyika
Mjini Njombe,Katibu Mkuu wa CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa Amesema Kupitia
Rasilimali Zilizopo Hapa Nchini Tanzanaia Ingeweza Kuwa Miongoni Mwa Mataifa
Matajiri Duniani,Lakini Kutokana na Kukosekana Kwa Viongozi Wenye Utashi wa
Kitaifa Bado Nchi Hii Imeendelea Kuwa Kati ya Mataifa Masikini Dunia.
Amesema Miongoni Mwa Mambo Yanayopaswa Kusimamiwa na
Serikali na Kuhakikisha Yanaboreshwa ni Pamoja na Miundombinu ya Elimu Badala
ya Kuwaachia Wananchi Mzigo wa Kuchangia Ujenzi Huo,Huku Pia Akiitaka Serikali
Kuboresha Sekta Kama Vile za Afya na Barabara.
Awali Akizungumza Kwenye Mkutano Huo Mbunge wa Nyamagana
Kwa Tiketi ya CHADEMA Ezekiah Wenje Amesema Serikali Imekuwa Ikipoteza Mapato
Mengi Kutokana na Misamaha ya Kodi Hivyo ni Vema Serikali Ikafikiria Namna Mpya
ya Kuweza Kudhibiti Mapato Yake Kutoka Kwa Wawekezaji
Mkutano Huo Pia Ulihudhuriwa na Viongozi Mbalimbali
Wakiwemo Wabunge wa Chama Hicho Akiwemo Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi
na Viongozi Wengine wa CHADEMA Wilayani Njombe
No comments:
Post a Comment