hawa
ni baadhi ya wazazi waliolalamikia kutumia migambo kuzunguka na
wanafunzi kwenda kuonesha nyumba zao kwa ajili ya michango ya chakula
shuleni.
Hawa
ni baadhi ya Wazazi waliolalamikia watoto wao kurudishwa na migambo
kuonesha nyumba zao ili kuchangia chakula April 16 mwaka huu.
Hapa
mwenyekiti wa kamati ya chakula katika shule ya msingi Mabatini Bwana
Edward Mlowe akimuonesha mwandishi wa mtandao huu bwana Gabriel kilamlya
orodha ya wazazi waliochangia chakula na wasiochangia huku baadhi ya
wazazi walioonekana kulalamikia tatizo hilo wakionekana kutochangia
kabisa kwa takribani awamu mbili,na wanaoonekana pembeni ni wazazi
waliokuwa wakipeleka chakula baada ya nguvu ya mgambo kutumika.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mabati Njombe Bi.Elizabeth
Mhonjwa akieleza kilichopelekea kutumia njia mbadala ya kuwatafuta
wazazi baada ya serikali ya mtaa kushindwa kufanikisha zoezi hilo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya chakula ya shule ya Msingi Mabatini bwana Edward Mlowe
akiandika jina lake kwenye Notebook ya Mwandishi wa Mtandao huu akiwa
ofisini kwa mwalimu mkuu wa Shule hiyo leo baada ya kutolea ufafanuzi wa
kilichopelekea kutumia nguvu mbadala ya kutafuta chakula.
Hapa
ni eneo la Shule la Nyuma ambako mwalimu mkuu wa shule hiyo amepanda
miti aina ya Parachichi takribani 20 kwa ajili ya Mradi wa Shule.
Baada
ya nguvu ya Mgambo kutumika kuwatafuta wazazi ambao hawjachangia
chakula shuleni hatimaye chakula chapatikana na kinapikwa ili wanafunzi
waendelee kula.
Mgambo
aliyetumika kuzunguka na watoto kwenda kuonesha nyumba zao ili kudai
michango ya chakula kwa wazazi baada ya serikali ya mtaa kushindwa
kuwapata wazazi huyu hapa.
Baadhi
ya wanafunzi wakipumzika mara baada ya kusaidia kusogeza huduma ya maji
na chakula kwa mpishi shuleni hapo mapema leo Asubuhi.
Hii
ni Shule ya Msingi Mabatini Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe ambako
yameibuka malalamiko kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wakidai uongozi
wa shule hiyo kuwafukuza shuleni kwenda na Mgambo kuonesha nyumba zao
kwa ajili ya kusaka michango ya chakula.
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mabatini wakisoma Nadharia kwa vitendo nje ya madarasa yao na mwalimu wao leo.
Huyu
ni Afisa mtendaji wa Mtaa wa SIDO na Buguruni Mjini Njombe Bi.Rehema
Ngailo akieleza uamuzi wa kamati ya shule kufikia hatua ya kutumia
mgambo kuwasaka wazazi nyumbani kwao.
Na Gabriel Kilamlya.
Kufuatia Malalamiko ya Baadhi ya Wazazi Wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini Mjini Njombe,Kulalamikia Kitendo Cha Uongozi wa Shule Hiyo Kuwafukuza Wanafunzi Kwa Madai ya Kukosa Michango ya Chakula,Uongozi wa Shule Hiyo na Serikali ya Mtaa wa SIDO Umeibuka na Kutolea Ufafanuzi Malalamiko Hayo ya Wazazi.
Wakizungumza ofisini kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo,Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula ya Shule Hiyo na Afisa Mtendaji wa Mitaa ya SIDO na Buguruni Wamesema Baadhi ya Wazazi Kwenye Shule Hiyo Wamekuwa Kikwazo Kwa Kukwamisha Mipango Mbalimbali ya
Rehema Ngailo ni Afisa Mtendaji wa Mitaa Hiyo Amesema Utaratibu wa Ukusanyaji Michango ya Shuleni ni Kwa Kupitia Kamati Ilioteuliwa na Uongozi wa Shule na Kuridhiwa na Wazazi Wote,Hivyo Kitendo Cha Baadhi ya Wazazi Kupinga Mpango Huenda Kimelenga Kurudisha Nyumba Maendeleo ya Shule Hiyo.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula Shuleni Hapo Bw Edward......Amesema Kutokana na Baadhi ya Wazazi Kuwa Wagumu Kuchangia Michango Hiyo,Uongozi wa Shule Hiyo Kwa Kushirikiana na Kamati ya Shule Umeamua Kuwatumia Mgambo Ili Kuweza Kukusnya Michango Hiyo na Kukanusha Madai Kuwa Watoto Hao Walifukuzwa Shuleni.
Awali Wakizungumza na www.michaelngilangwa.blogspot.com,Baadhi ya Wazazi Hao Waliutupia Lawama Uongozi wa Shule ya Msingi Mabatini Kwa Uamuzi Wake wa Kuwafukuza Shuleni Wanafunzi 25 Kwa Madai ya Kukosa Michango ya Chakula,Jambo Ambalo Walidai Kuwa Huenda Lingewaathiri Kitaaluma.
Kumekuwa na Jitihada Mbalimbali Zinazofanywa na Serikali Kuhimiza Umuhimu wa Chakula Cha Mchana Shule,Ingawa Jitihada Hizo Pia Zimekuwa Zikikumbana na Changamoto Mbalimbali.
.........................................................................................................................
No comments:
Post a Comment