Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, April 20, 2013

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMBAKA BINTI MWENYE MIAKA 17 NJOMBE

.
Na Michael Ngilangwa Njombe.

Mkazi Mmoja wa Mtaa wa Kahawa Makambako Mkoani Njombe Leo Amefikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe Akituhumiwa Kwa Kosa la Kumbaka Binti Mwenye Umri wa Miaka Kumi na Misaba.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Serapian Matiku Ameambia Mahakama Hiyo Kuwa Kati ya Dec Mosi na Dec 30 Mwaka 2012 Mtuhumiwa Alidaiwa Kumbaka Binti Huyo Katika Mtaa wa Ikwete B Makambako Mkoani Hapa.

Bw .Matiku Ameiambia Mahakama Hiyo Kuwa

Kosa Hilo ni Kinyume na kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili {E} na kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu sura ya 16 volimu ya kwanza kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kesi Hiyo Inayosikilizwa Chini ya Hakimu John Kapokolo Imeahirishwa Hadi June 20 Mwaka Huu Kutokana na Kutokamilika Kwa Upelelezi Huku Mtuhumiwa Akikana Kuhusika na Tukio Hilo na Kwa Sasa Akiwa Nje kwa Dhamana Baada ya Kutimiza Masharti ya Kuwa na Wadhamini Wawili Walioweka Dhamana ya Shilingi Millioni Mbili Kila Mmoja.


 

Wakati Huo Huo Mahakama ya Wilaya ya Njombe Imemuachia Huru Mkazi Mmoja wa Kijiji Cha Lwangu Wilayani Njombe Alex Kadege Aliekuwa Akituhumiwa Kwa Kosa la Kujipatia Mali Kwa Njia ya Udanganyifu.

Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Amesema Kutokana na Mlalamikaji Kushindwa Kuwasilisha Vielelezo Mahakamani Hapo Jambo Linalofanya Shauri Hilo Kukosa Nguvu ya Kisheria,Mahakama Imeamua Kumuachia Huru Mtuhumiwa na Kusema Kuwa Rufaa Iko Wazi Kwa Mlalamikaji.

Awali Akisoma Hati ya Mashtaka Mahakamani Hapo Mwendesha Mashtaka wa Polisi Serapian Matiku Ameaimbia Mahakama Kuwa Mnamo
april 26 mwaka 2012  majira ya saa tatu asubuhi akiwa kijiji cha lwangu  alidanganya kwamba anachukua pikipiki aina ya T Better yenye  namba za usajili T 959 yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne mali ya Fotenatus Muhamilawa akidai anakwenda kuchukua mafundi kijiji cha Ihanga na Kisha kwenda kuiuza katika kijiji cha Igagala.

No comments:

Post a Comment