Saturday, April 13, 2013
MBUNGE WA NJOMBE KASKAZINI deo sanga AWARIDHISHA VIJANA WA KATA MBALIMBALI ZA JIMBO LAKE KWA KUHAMASISHA MICHEZO NA KUGAWA VIFAA VYA MICHEZO.
Diwani wa kata ya Mfriga akipokea pia vifaa vya michezo kwaajiliya vijana wa kata hiyo.
Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akiwa ameongozana na Mbunge wa Njombe Kaskazini.
Diwani Wa kata ya Lupembe Bi wapalila akipokea vifaa vya michezo kwaajili ya vijana wa kata yake.
Hapa ni kata ya kidegembye vijana wanakabidhiwa jez na mipira licha ya wananchi kutofurahishwa na uongozi wa kata na kijiji cha Kidegembye kwa kushindwa kutatua matatizo yao yanayowakabili huku wakishangazwa na bati 40 zilizotolewa na Mbunge huyo kutowekwa wazi na viongozi hao.
Wananchi mara tu Mbunge aliposimama na kusema hapa ni lileta bati 40 kwaajili ya zahanati wananchi walisema tunashangazwa kuona unatwambia ulileta bati sahizi mbona viongozi wetu waliuza msitu wa kijiji ndipo wakanunua bati za ukalabati wa zahanati hiyo kumbe nawe ulitoa.
Vijana wa jimbo la Njombe kaskazini wame nufaika na msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jez ambazo zilitolewa na Mbunge wao Deo Sanga wakati akitembelea jimbo lake katika vijiji na nkata zake.
Zawadi za vifaa hivyo vya michezo vimetolewa kufuatia maombi yalikuwa yakitolewa na vijana mbalimbali wa kata na vijiji alivyokuwa akitembelea mbunge huyo na hivyo alikuwa anatimiza ahadi zake.
Pamoja na kuwa vijana hao walinufaika na kupatiwa vifaa vya michezo hivyo lakini imekuwa ngumu kwa wasichana kupatiwa vifaa hivyo hususani vifaa aina ya jez kuwa hazipatikani dukani kiurahisi rabda mpaka zikashoneshwe hali ambayo wasichana wameona itachukua muda mrefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment