Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, April 13, 2013

MBUNGE WA NJOMBE KASKAZINI AKUTANA NA CHANGAMOTO YA KUHARIBIKA KWA GARI LAKE LA MATANGAZO LUPEMBE,WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO WAWASUMBUA WAKULIMA LUPEMBE.





Wanyama waharibifu wanaowasumbua wakulima wa lupembe  katika mazao yao ya mahindi msimu huu na hapa ni jitihada zao wakulima kuwawinda na kuwauwa kwa kutumia zana na jadi.









Hali halisi ilikuwa hivi hili ni gari la Mbunge la matangazo limeharibika akiwa njiani akielekea kijiji cha ukalawa.





Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea jimbo lake la Njombe kaskazini aliweza kukabiliana na changamoto kama hivi barabarani.Picha Na Michael Ngilangwa.

Kikwazo kikubwa alichokumbana nacho Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga ni kuharibika kwa gari lake wakati akielekea kijiji cha Ukalawa njiani gari lake la matangazo liliharibika hali iliyompelekea kuchelewa kufika eneo la tukio licha ya wananchi kusubiria kwa muda mrefu pasipo kutokea.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo za kuharibika kwa gari lake la matangazo ambalo lilimsaidia sana kupaza sauti wakati akiwahutubia wananchi wake waweze kumsikia vizuri anachokizungumza lilipoharibika ikamrazimu aende pasipo kuwa na gari lenye spika za kupazia sauti katika kijiji cha ukalawa.

Safari yake haikuweza kusitishwa lakini ilifanikiwa mpaka mwisho alipomaliza ziara yake april 8 mwaka huu na kuwa shukuru wananchi kwa mapokeo yao mazuri.

Lakini wakti akienda kutembelea vijiji na kata za jimbo hilo wananchi wa Lupembe kilio chao kikubwa kilikuwa ni wanyama waharibifu ambao maafisa maliasili kuahidi kwenda kuwafukuza tarehe 15 mwezi huu.

No comments:

Post a Comment