Bunge la kumi la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linaendelea
mjini Dodoma huku likiwa limepanda joto kali kutokana na changamoto za matumizi
ya lugha.
Leo asubuhi mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya
chama cha mapinduzi (CCM) Deo Filikunjombe amekutana na kikwazo cha kiti cha spika wa bunge Anne Makinda baada ya kutumia maneno ambayo yalionekana kuwa sio ya kibunge.
chama cha mapinduzi (CCM) Deo Filikunjombe amekutana na kikwazo cha kiti cha spika wa bunge Anne Makinda baada ya kutumia maneno ambayo yalionekana kuwa sio ya kibunge.
Filikunjombe alisema, “Mi nianze kusema bayana kwamba mi
siungi mkono hoja kwa asilimia 100 kwa sababu zifuatazo, siungi mkono hoja kwa
sababu kila anaeona atakuwa shahidi kuwa serikali yetu imekuwa sio serikali
sikivu kwa vitendo,na serikali yetu imekuwa na tabia ya kufunika kombe ili
mwanaharamu apite, siungi mkono hoja kwa sababu serikali yetu imevaa miwani ya
mbao na imeziba masikio.”
Hata hivyo spika wa bunge hilo alimkatisha Filikunjombe na
kumtaka aondoe maneno aliyosema ‘serikali imevaa miwani ya mbao’, na mbunge
huyo alifanya hivyo na kusisitiza kuwa serikali sio sikivu na imeziba masikio.
Mbunge huyo aliongeza kuwa mawaziri wa serikali wamekuwa
wakilindana na kwamba mawaziri wanaowajibika ni wachache na wanaweza wakawa
kumi tu kati ya idadi kubwa ya mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Pia alitoa wito kwa wabunge wa chama cha mapinduzi
kubadilika na kuacha kubeza kila hoja za wapinzani, “waheshimiwa wabunge
wenzangu hasa sisi wa chama tawala, ifike mahala tuache kubeza kila hoja za
wapinzani, tusiwabeze badala yake tuchukue hoja zao tuzipime na tuzifanyie
kazi.”
Mwakilishi huyo wa wananchi wa jimbo la Ludewa alimaliza kwa
kutaja mahitaji muhimu ya jimboni kwake kuwa ni vitu vichache kama meli, na
meli zilizopo kama MV Songea na MV Iringa ni mbovu na hazifanyi kazi, ukosefu
wa barabara ya lami, na kutokuwepo kwa chuo cha VETA, na kwamba kama hawatapata
huduma hizo muhimu na wao pia watakwenda kuandamana barabarani wakiwa na sare
zao za kijani bila kujali kuwa ni siku ya jumatatu, ijumaa au ni jumapili.
chanzo leotainmentblogu.
No comments:
Post a Comment