Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, March 25, 2013

WASIOCHANGIA UJENZI WA SHULE ZA MSINGI NJOMBE KUPELEKWA BARAZA LA KATA SASA.

 Diwani wa kata ya Njombe mjini wa pili toka kushoto Mhe.Lupyana Fute[JACKY'S]anayefuatia ni afisa mtendaji wa kata ya Njombe mjini bwana Donard Mng'ong'o na mwishoni kulia ni mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ya msingi Ruhiji B bwana Zephania Msigwa ikiwa aliyesimama ni mwenyekiti wa mtaa wa Gwivaha mjini Njombe.
 WANANCHI Wakiwa makini kusikiliza mkutano wa hadhara uliofanyika jana ukiwataka wazazi kuchangia mchango wa ujenzi wa shule ya msingi Ruhuji B kiasi cha shilingi elfu 30 kwa kila kichwa.
 Hili ni jengo jipya lenye madarasa manne lililojengwa kwa miezi Minne hadi sasa kutokana na usimamizi na mchango mkubwa wa wafanyabiashara mjini Njombe ikiwa hadi hatua hiyo zaidi ya shilingi milioni 26 zimeshatumika.
 Huyu ni afisa wa afya ambaye ni muuguzi wa wagonjwa wa HIV majumbani mjini Njombe akitoa maelekezo juu ya wagonjwa kufika kwake wakiwa na kadi zao ili kupata dawa.
 Donard Mng'ong'o  ambaye ni Afisa mtendaji wa kata ya Njombe Mjini aliyesimama akizungumzia juu ya hali ya wananchi kushindwa kujitokeza kwenye mikutano ya hadhara na kisha kuanza kulalamika.
 Diwani wa kata ya Njombe Mjini Mh. Lupyana Fute akisema hakuna mzaha kwa yule ambaye hajachangia kinachofuatia ni faini tu.
 Hii ni shule ya msingi Ruhuji ya sasa ambayo bado majengo yake hayatoshi na tayari zaidi ya wanafunzi 100 wamejazana katika darasa moja shule inayohitaji msaada wa kupunguziwa wanafunzi mjini Njombe.
SHULE YA Msingi Ruhuji mjini Njombe .

Uongozi wa Kata ya Njombe Mjini Umesema Utawakamata na Kuwafikisha Mbele ya Baraza la Kata Hiyo Pamoja na Kuwashtaki na Kuwachukulia Hatua za Kisheria Wazazi Saba Walioshindwa Kuchangia Chakula Kwa Watoto Wao.

Aidha Uongozi Huo Pia Umewataka Wazazi Kuendelea Kuchangia Michango Kwa Ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Ruhuji na Idundilanga Ambazo Ujenzi Wake Umekuwa Ukiendelea Kupitia Michango ya Wananchi.

Akizungumza Wakati wa Mkutano wa Kusoma Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Michango Kwa Ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Ruhuji,Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kwivaha Bw
Brayson Lupenza Amesema Hadi Kufikia Mwitikio wa Wananchi wa Mtaa Huo Kuchagia Ujenzi wa Shule Hiyo ni Mdogo Ikilinganishwa na Idadi ya Wananchi Waliotegemewa Kuchangia

Amesema Kati ya Wakazi 900 wa Mtaa Huo Waliotakiwa Kuchangia Wakati 482 Tu Ndio Waliochangia Huku 499  Wakishindwa Kuchangia Hadi Sasa Hatua Inayoulazimu Uongozi wa Mtaa Huo Kuwataka Kuchangia Kabla Hatua za Kisheria Hazijachukuliwa Dhidi Yao.

Amezitaja changamoto zilizopelekea kutofanikisha ukusanyaji wa michango hiyo kuwa ni pamoja na wananchi kutoa lugha za matusi kwa wachangishaji kuwakimbia na kujifungia pindi wachangishaji wanapo pita kuchangisha michango hiyo.

Kwa Upande Wake Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Bw Lupyana Fute Amesema Pamoja na Hatua ya Kuwashtaki Wananchi Watakaoshindwa Kuchangia Michango Hiyo Pia Uongozi Wake Hautomfumbia Macho Afisa Yoyote wa Mtaa Atakaeonekana Kutaka Kukwamisha Zoezi Hilo.

No comments:

Post a Comment