BAADA YA HAPO BURUDANI YA NYIMBO MBALIMBALI IKIWEMO NGOMA TOKA KIJIJI CHA LYALALO WAKAANZA KUTUMBWIZA PAMOJA NA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA MANYUNYU.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Manyunyu iliyopo tarafa ya Lupembe wilayani Njombe wakiwa pamoja na wananchi kwenye maadhimisho hayo siku ya jana.
Wananchi wakiburudisha wakati wa maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani jana Katibu Tawala wilaya ya Njombe Evagray Keiya akisoma hotuba mbele ya wananchi wa kijiji cha Matembwe wilayani Njombe.
MKURUGENZI HALMASHAURI YA MAKAMBAKO AKITOA SALAAM KWA WANANCHI WA MATEMBWE.
DIWANI WA KATA YA MDANDU ANA UPENDO GOMBELA AKITOA SALAAM PIA.
KAIM MGANGA MKUU HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE DR CONRAD UGONILE .
NGOMA YA ASILI TOKA LYALALO WAKIINGIA UWANJANI KUBURUDISHA MBELE YA MGENI RASMI.
Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Njombe Paulo Malala nae avutiwa na ngoma ya lingapulila.PICHA NA MICHAEL NGILANGWA.
Miongoni Mwa Tahadhari Zilizopendekezwa ni Pamoja na Wananchi Kuhepuka Misongamano Isio ya Lazima,Kuishi Kwenye Nyumba Zinazoruhusu Hewa na Kutotema Mate Hovyo.
Akizungumza Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani Yaliofanyika Jana Katika Kijiji Cha Matembwe Wilayani Njombe,Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Bw Evagrey Keiya Amesema
Serikali Imeendelea Kuboresha Huduma za Afya Kwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu Kwa Kuhakikisha Vipimo na Dawa Zinapatikana Katika Vituo Vinavyotoa Huduma Hiyo.
Amesema Kwa Kuzingatia Takwimu za Idara ya Afya,Asilimia 60 ya Wagonjwa wa Kifua Kikuu Wana Maammbukzi ya Virusi Vya UKIMWI Jambo Linaloashiria Ukubwa wa Tatizo Hilo Wilayani Njombe na Hivyo Kusisitiza Umuhimu wa Wananchi Kuwahi Tiba Kwa Kuwa Ugonjwa Huo Unatibika.
Awali Akisoma Taarifa ya Hali ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu Wilayani Njombe,Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Dokta Konrad Ugonile Amesema Kipindi Cha Miaka Minne Kutoka Mwaka 2009 Hadi Mwaka 2012 Kumekuwa na Ongezeko la Wagonjwa wa Kifua Kikuu Wilayani Njombe Jambo Linaloifanya Wilaya ya Njombe Kuwa Miongoni Mwa Wilaya Zinazoripoti Vifo Vingi Vinavyotokana na Ugonjwa Huo Kwa Mwaka.
Amesema Mwaka 2009 Wagonjwa Waliogundulika Kuwa na Kifua Kikuu Walikuwa 286,,Mwaka 2010 Wagonjwa 354,Mwaka 2011 Wagonjwa 397 na Mwaka 2012 Wagonjwa 433.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ina Jumla ya Vituo 65 Vya Ugunduzi wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu Katika Kata za Kipengere,Ilembula Hospitali,Lupembe,Kidugala,Wanging'ombe,Makambako,Matembwe na Hospitali ya St Joseph Ikelu.
Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Huadhimishwa March 24 Kila Mwaka Duniani Kote Yakiwa na Lengo la Kuongeza Mapambano Dhidi ya Ugonjwa Huo.
No comments:
Post a Comment