Tuesday, March 19, 2013
SAKATA LA KUBINAFSISHWA KWA EKARI 16 ZA KIJIJI CHA MASAULWA LA FIKIA HATIMA BAADA YA VIONGOZI WA KIJIJI HICHO KUKILI KULIPA PESA KWA MUWEKEZAJI PAMOJA NA RIBA NA ARDHI IRUDI KUWA MALI YA KIJIJI.
Mwenyekiti wa kijiji cha Masaulwa Elias Mgaya akizungumza na wananchi wa kijiji cha masaulwa na kukili serikali ya kijiji kulipa deni la fedha shilingi milioni moja na laki tano.
Wajumbe wa halmashauri ya kijiji cha Masaulwa wakiongozwa na mwenyekiti wao Elias Mgaya.
Diwani kata ya Imalinyi Enock Kiswaga akizungumza na wananchi wake na kusema uongozi unatakiwa kuwajibika kulipa deni hilo kwa kuwa walifanya uamuzi pasipo kuwashirikisha wananchi.
wananchi wa kijiji cha Masaulwa wakiwa kwenye mkutano huo
Afisa mtendaji wa kijiji hicho akijitetea kuhusu kuishi mbali na mahala pa kazi baada ya diwani wa kta hiyo kutoa amri ya yeye kuishi katika kijiji hicho kwakuwa wananchi walimjengea nyumba ya kuishi.
Sakata la Wananchi wa Kijiji Cha Masaulwa Kata ya Imalinyi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Kumkataa Mwekezaji Aliemilikishwa Ardhi ya Kijiji Hicho Kinyume Cha Utaratibu,Limeingia Kwenye Sura Mpya Baada ya Uongozi wa Kijiji Kukubali Kurudisha Fedha Kiasi Cha Shilingi Millioni Moja na laki tano Ilizochukua Kutoka Kwa Mwekezaji Huyo.
Akizungumza Mbele ya Mkutano wa Hadhara na Wananchi wa Kijiji Hicho Mwenyekiti wa Kijiji Cha Masaulwa Bw Elias Mgaya Amesema Pamoja na Kukubali Kurudisha Fedha Hizo Pia Uongozi Mzima wa Kijiji Akiwemo Afisa Mtendaji na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji Watapaswa Kuwajibika.
Uamuzi Huo wa Serikali ya Kijiji Cha Masaulwa Unakuja Ikiwa ni Siku Chache Baada ya Wananchi wa Kijiji Hicho Kulalamikia Uongozi wa Kijiji Kumilikisha Hekari 16 za Kijiji Kwa Mwekezaji Bila Ridhaa ya Wananchi.
Enock Kiswaga ni Diwani wa Kata ya Imalinyi Anawapomgeza Wananchi Kwa Ujasiri wa Kusimamia Haki Yao na Kuwataka Viongozi wa Vijiji Kuwashirikisha Wananchi Pindi Wanapotaka Kufanya Makubaliano Yoyote Yanayohusu Mali za Umma.
Kurudishwa Kwa Fedha Hizo Kiasi Cha Shilingi Millioni Moja na laki tano ikichanganywa na riba Kwa Mwekezaji Huyo Kunafanya Ardhi Hiyo Kurudi Kwa Wananchi na Kutoa Nafasi Kwa Wananchi Kuweza Kuitumia Kwa Shughuli Mbalimbali Hasa Zile za Kilimo.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Imalinyi Wilayani Wanging'ombe Bw Enock Kiswaga Amemtaka Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Masaulwa Bw Samwel Masawa Kuhakikisha Anaweka Makazi Yake ya Kudumu Kijijini Hapo Badala ya Kuondoka Mara Kwa Mara Kama Ilivyo Sasa.
Aidha Kitendo Cha Mtendaji Huyo Kuondoka Mara Kwa Mara Kimelalamikiwa na Wananchi Kwa Madai ya Kuzorotesha Jitihada za Kimaendeleo za Kijiji Hicho.
Akizungumza Wakati wa Mkutano wa Hadhara na Wananchi Pamoja na Mtendaji Huyo Bw Kiswaga Amesema Kwa Kuwa Uongozi wa Kijiji Uliamua Kumjengea Nyumba Mtendaji Huyo Hivyo Hakuna Sababu ya Yeye Kutoishi Kijijini Hapo.
Akizungumza Kwenye Mkutano Huo, Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Masaulwa Bw Samweli Masawa, Amesema Miongoni Mwa Sababu Zinazosababisha Kutoishi Kijijini Hapo na Kutoitumia Nyumba Hiyo ni Pamoja na Nyumba Kutokamilika Baadhi ya Miundombinu Ikiwemo Maji na Choo.
Hata Hivyo Wananchi Hawakukubaliana na Sababu Hizo, Kwa Madai Kuwa Nyumba Hiyo Ilikamilika Mapema, Isipokuwa Mtendaji Huyo Amekuwa na Mazoea ya Kuwa Nje na Kituo Chake Cha Kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment