Hili ni shimo lililopo eneo la Sambala mjini Iringa barabara ya Iringa - Dodoma
Hapa ni eneo la Kihesa sokoni barabara ya Iringa - Dodoma
Kihesa mjini Iringa
Hapa ni Eneo la Makosa mjini Iringa karibu kabisa na ofisi za Manispaa ya Iringa
Hapa ni eneo la Sabasaba mjini Iringa Bajaji ikiwa imeharibika baada ya kuingia katika shimo
Eneo la Manispaa ya Iringa hapa
Sambara mjini Iringa
Manispaa ya Iringa hapa unaona shimo hili
Kihesa eneo la Majembe
Eneo la Nationali mjini Iringa hapa
Kihesa sokoni hapa
Eneo la Sambala mjini Iringa
Tanroads mpo ama mmelala ?
RC Iringa Dkt Christina Ishengoma upo ?
Meneja wa TANROADS mkoa Paul Lyakurwa (kushoto ) akimpokea waziri
mkuu Mizengo Pinda ,wa kwanza kushoto ni katibu wa mbunge jimbo la
Ismani Thom Malenga
Shimo eneo la Mwang'ingo mjini Iringa
Hapa si kijijini ni Iringa mjini
Kihesa mjini Iringa na hii ni barabara ya mkoa wa Iringa si kijiji ,inangoja ziara ya viongozi wa kitaifa ndipo itengenezwe
Barabara kibogoyo mjini Iringa umepata kuona ?
Hili shimo lipo nje ya ofisi ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kama kwa mwakilishi wetu ni hivi
Hali ya barabara ya mkoa wa Iringa ,barabara ya Iringa -Dodoma
kuanzia eneo la Samora hadi Kihesa kilolo katika Manispaa ya Iringa
ambayo ni sura ya mkoa wa Iringa ni mbaya na inayosikitisha na hata
kuchafua mwonekano wa mkoa wa Iringa kwa ujumla.
Yawezekana zipo sababu zinazopelekea kuwepo kwa ubovu huo wa barabara sababu ambazo uongozi wa wakala wa barabara mkoa wa Iringa TANROADS unazijua ila yawezekana pia sababu hizo hazikubaliki kwa watumiaji wa barabara hiyo hasa ukizingatia kuwa maeneo ambayo barabara hiyo imechakaa kupita kiasi ndio sura ya mkoa mzima.
Binafsi imenichukua muda wa zaidi ya miezi miwili sasa kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu kuhusu TANROADS mkoa wa Iringa inavyofanya kusudi kuendelea kuacha barabara hii nyeti kwa sura ya mkoa wetu ikiendelea kuharibika bila kuchukua hatua za kuziba japo mapengo yanayoendelea kuitesa barabara hii ya Iringa - Dodoma katikati ya mji wa Iringa.
Si wakati wa kuwafundisha kazi viongozi wa TANROADS mkoa wa Iringa wala mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa na mkuu wangu wa mkoa Dkt Christina Ishengoma kuhusu kero hii ya barabara ndani ya mji wa Iringa.
Ila ni wakati wa kuwaomba viongozi wangu hawa kwa maana ya wakala wa barabara mkoa wa Iringa Injinia Msomi Paul Lyakurwa ambae ni meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa , mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba na mkuu wangu wa mkoa Dkt Ishengoma kutoka ofisini na kusaidia msaada wa meno kwa kibogoyo huyu barabara ya Iringa - Dodoma.
Zamani nilikuwa nikishuhudia wananchi wa vijijini ndio ambao walikuwa wakilalamikia ubovu wa barabara ila leo katika karne hii ya sayansi na Teknolojia tunashuhudia mapengo ya barabara yanatesa mjini ambako viongozi wote wapo.
Binafsi siamini kama ajali zinazotokea katika mji wa Iringa zinasababishwa na uzembe wa madereva ila ninachoamini ajali hizi zinasababishwa na uwajibikaji mbovu wa wenye mamlaka waliopewa kusimamia barabara hii na hata kuacha barabara kuwa na mashimo makubwa kama haya .
Barabara za mji wa Iringa ni chakavu sana na mbaya zaidi kwa sasa ubovu huo umesogea hadi katika ofisi ya mbunge Mchungaji Peter Msigwa ambae ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Iringa mjini ila pia bila aibu mashimo yamesogea hadi katika mlango wa mkuu wa mkoa wa Iringa ambapo katika lango lake kuna mashimo ambayo naweza kusema ni mashimo ya karibu wageni ofisi ya RC Iringa.
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wakati ukiandaa ripoti hii ulitaka kupita barabara ya Pawaga Road ili kuona barabara ya mbunge na mkuu wa mkoa ikoje na kuona pia kuna shida .
Haya ni maeneo ambayo yameathirika kupita kiasi na bila shaka uongozi wa barabara mkoa wa Iringa unasubiri ziara ya viongozi wa kitaifa ili kufanya kazi usiku na machana kuziba mashimo haya ambayo kweli yanaifanya serikali iliyopo madarakani kuendelea kuchukiwa zaidi na wapiga kura wake achiliambali mbunge wa jimbo ambae yeye ni mkazi wa Iringa na anashuhudia ubovu huu.
Uchunguzi unaonyesha kuwa eneo la Nationali mjini Iringa limeharibika vibaya , eneo la Zebra ,eneo la Tanesco , eneo la ofisi ya mbunge wa Iringa mjini ,eneo la ofisi ya RC Iringa , eneo la Makosa , TFA , Sabasaba , Sambala , FFU, Kihesa na Mwang'ingo ndio ambayo ni hatari zaidi kwa usalama wa watumiaji wa vyombo vya moto kwani mashimo ni makubwa zaidi na iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa ajali katika mji wa Iringa si chanzo cha madereva bali ni uzembe wa TANROADS kushindwa kuchukua hatua zaidi .
Zipo sababu kuwa eti barabara hiyo inatengenezwa na wachina kutoka Iringa - Dodoma ila kasi yake ni ndogo zaidi na hata kama hivyo bado wakati tunasubiri ujenzi huo ni vema ukarabati uwepo.
...........................................ITAENDELEA WIKI IJAYO .......................................

No comments:
Post a Comment