Huyu ndie mhubiri maarufu wa
kimataifa kutoka Afrika ya kusini ambae yupo kushusha neema ya maombi
kwa wakazi wa mkoa wa Iringa anaitwa nabii Joshua Cyrill
Mhubiri maarufu kutoka nchini Kenya
mtume Bonface Indeche ambae pia amekuwa ngunzo kubwa mkoani Iringa kwa
hutuma yake nzuri ya kihoro anayoendelea kuitoa
Kama
ni vita mbaya ambayo inaweza kupoteza heshima ya kiroho mkoni
Iringa ni pamoja na mbinu chafu zilizojitokeza siku za hivi karibuni
kwa baadhi ya wahubiri mkoani hapa kuendekeza uchoyo wa kihoro na
kutaka kuendelea kuhubiri wenyewe na sio wengine .
Uchunguzi
wa kina uliofanywa na mtandao wa
www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwepo kwa vita kubwa kati ya
baadhi ya wahubiri wa makanisa haya yaliyoanza kuchipuka siku za
hivi karibuni kwa kuwazuia wahubiri wengine kuifanya huduma hiyo
ndani ya mkoa wa Iringa.
Majina
ya wahubiri hao ambao wanaendekeza uchoyo wa Kiroho kwa sasa
yamewekwa kapuni na mtandao huu ,ila hali iliyofikiwa ni mbaya na iwapo
suala hili litaendelea kunyamaziwa upo uwezekano mkubwa wa
heshima na sifa ya viongozi wa dini ikatoweka na waumini wao kuanza
kuhoji mengi juu ya hali hiyo.
Mtandao
huu umekuwa ukifuatilia picha nzima ya vita hiyo inayoendelea na
kuna njama zinazopangwa za kuendelea kuwaharibia wahubiri hao japo
wakazi wa mjini Iringa wametokea kuwapongeza kwa ujio wao ndani ya
mkoa wa Iringa wenye tatizo kubwa la UKIMWI na kutaka wahubiri
wenyeji wa makanisa hayo kuacha wivu wa huduma na badala yake
kujipanga upya na kuwapa ushirikiano wageni hao .
wahubiria
hao ambao walipangwa kuanza semina ya neno ya Mungu kuanzia Machi
21 mwaka huu katika ukumbi wa Embakasy Ilala wamezuiwa kufanya
hivyo baada ya mhubiri mmoja kudaiwa kutumika kuwavuruga wahubiri
hao
...........Usikose kuendelea kufuatilia undani wa sakata hili hapa ................
No comments:
Post a Comment