Wataalamu wa Maji kutoka Halmashauri ya
Mji wa Njombe wakiwa kwenye picha ya Pamoja mara baada ya kuwekwa jiwe
la msingi la mradi wa maji katika kijiji cha Mgala leo.
Mtaalamu wa kutibu maji toka
halmashauri ya mji wa Njombe akinawa mikono kwenye maji ya mtiririko
kutoka kwenye bomba linaloonekana hapo juu.
Afisa kilimo wa kata ya Ihanga bwana
Onesmo Kamonga kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo bwana Rainard Kigola
ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi
wa maji wa kijiji cha Mgala utakao hudumia zaidi ya wakazi 400.
Wakati wengine Njombe wakilia na Uhaba mkubwa wa maji wengine wafurahia na kuchezea maji hayo huko Mgala.
Huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Mgala
bwana Donatus Mmero akizungumza na wananchi akiwapongeza kwa kufanikisha
kuwekwa kwa jiwe la msingi mradi wa maji kijijini humo.
Wengine hakuna shida ya maji kabisa na wengine kilio cha uhaba wa maji katika mkoa Mmoja wa Njombe.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kuelekea kilele cha wiki ya maji ya 25 inayofikia kilele chake machi 22 mwaka huu katika maeneo mbalimbali nchini
uchomaji moto na kusababisha kukausha vyanzo vya maji kukitajwa kusababishwa na kulipizana visasi miongoni mwa jamii.
Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa kata ya Ihanga bwana Onesmo Kamonga kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo bwana Rainard Kigola ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi wa maji wa kijiji cha Mgala utakao hudumia zaidi ya wakazi 400.
Bwana Kamonga amesema kitendo cha kulipizana kisasi kwa kuchoma moto mazingira athari yake si kwa mtu mmoja tu bali ni kwa jamii nzima baada ya kuharibika na kukauka kwa vyanzo vya maji.
Akisoma taarifa ya mradi wa maji hayo katibu wa kamati ya maji katika kijiji cha Mgala bwana Charles Mfugale amesema kuwa mara baada ya kuibuliwa kwa mradi huo mwaka 2010 hatua ya upembuzi yakinifu ikafanyika na kisha kulikabidhi kanisa katholic parokia ya Ihanga inayotekeleza mradi huo.
Aidha amesema kwa mujibu wa mkataba wa mradi huo mwezi juni mwaka huu unatakiwa uwe umekamilika na kisha jamii kutumia maji hayo huku wananchi wakitakiwa kuongeza kasi ya uchangiaji wa maji hayo kwa kutunza fedha itakayowasaidia endapo miundombinu itaharibika.
Machi 22 mwaka huu ni kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza machi 16 mwaka huu huku mkuu wa wilaya ya Njombe akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele hicho kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji kijijini Igominyi ambako halmashauri ya mji itaazimisha huko.
No comments:
Post a Comment