Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, March 14, 2013

NJOMBE MJI FC YAIGARAGAZA MATALAWE FC TATU BILA.


 Timu ya Njombe mji fc wakiwa ndani ya uwanja wa sabasaba katika mechi ya kirafiki.

 Timu ya Matalawe fc ndani ya uwanja wa sabasaba .

Mvua nayo ikasababisha mchezo kuwa mgumu kwa timu zote mbili. picha Na Michael Ngilangwa.



Katika mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Njombe  mji na Matalawe fc umetia hamasa kwa wapenzi na mashabiki wa timu ya Njombe mji baada ya kuibuka kidedea kwa kuifunga Timu ya Matalawe fc tatu kwa bila katika uwanja wa sabasaba uliofanyika jana jioni.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta ni kuvute Timu ya Njombe mji ilianza kupata neema katika kipindi cha kwanza baada ya kujipatia magori mawili kupitia washambuliaji wao madhubuti kabisa jezi nambari 10 Musa Maginga kuiandikia timu ya Njombe mji Gori la kwanza.

Gori la pili liliwekwa kinywani na mchezaji Bope Abdalah aliyepata pasi nzuri toka kwa mchezaji jezi nambari sita na hatimae akaweza kuona lango la timu ya Matalawe fc kipindi cha kwanza .

Hadi muamuzi anapuliza kipyenga akiashiria muda wa mapumziko timu ya matalawe ilikuwa haijaambulia kitu huku Njombe Mji ikitoka na magori mawili.

Baada ya kurejea uwanjani toka mapumziko mafupi timu ya matalawe ilijaribu kufurukuta kwa hali na mali iweze kujipatia gori walao la kufutia machozi lakini timu ya Njombe mji ilisema hapana kwa kupachika gori la tatu kupitia mchezaji wake Ebby Udope aliyekwenda kuliona lango la timu ya Matalawe fc.

Hadi mchezo unakwisha timu ya Njombe mji ilikuwa na magori matatu wakati matalawe ikitoka bila kitu.


No comments:

Post a Comment