Diwani wa kata ya Utengule Erasto Ngota akitoka ofisini kwake mara baada ya kuzungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com juu ya tuhuma za kushindwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara.
Mratibu elimu wa kata ya Utengule
Atirio Mveyange akichangia kuwa wananchi kushindwa kusomewa hesabu za mapato na matumizi ni kinyume na sheria za serikali.
Tofali zilizotelekezwa kijijini
Ngamanga baada ya serikali hiyo kushindwa kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo nyumba za walimu na zahanati.
Hizi ni tofali katika kijiji cha Ngamanga ambazo zina miaka zaidi mitano sasa bila kutumika kutokana na kuzitelekeza.
Diwani wa kata ya Utengule Mh.Erasto Ngota akiwa na mratibu elimu wa kata na msaidizi wake mwanamke huyo ofisini leo.
Hii ni barabara ya Utengule kuelekea kijiji cha Ngamanga inayotupiwa
lawama na wananchi kwa Mh.Diwani kushindwa kutekeleza ahadi yake ya
ujenzi wa barabara hiyo.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Diwani wa Kata ya Utengule Bw Erasto Ngota Amesema Kitendo Cha Wananchi Kuikataa Taarifa Hiyo na Kutishia Kufanya Maandamano ni Ishara Kuwa Uongozi wa Kijiji Umeshindwa Kuongoza Hivyo Wanatarajia Kufanya Mkutano Wiki Ijayo Ili Kuangalia Namna ya Kuuwajibisha Uongozi Huo Ikiwezekana Kuutoa Madarakani.
Amesema Katika Mkutano Huo Wanatarajia Kupokea Mapendekezo ya Wananchi Kama Wanataka Kuendelea na Uongozi Uliopo Madarakani Au Kuubadilisha Kulingana na Namna Uongozi Huo Ulivyosimamia Maendeleo ya Kijiji Hicho
Katika Hatua Nyingine Bw Ngota Amekiri Kuwepo Kwa Malalamiko ya Wananchi Yanayotokana na Kero Mbalimbali Zikiwemo za Ubovu wa Barabara,Ukosefu wa Huduma za Afya za Uhakika na Tatizo la Maji.
Mwishoni Mwa Wiki Iliopita Wananchi wa Kijiji Cha Ngamanga Waliikataa Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kijiji Hicho Ikiwa ni Katika Kile Walichodai Kuwa ni Dosari Kadhaa Zilizopo Kwenye Taarifa Hiyo.
Kufuatia Hali Hiyo Wananchi Hao Waliamua Kuchukua Hatua Mbalimbali Zikiwemo Kufunga Ofisi za Serikali ya Kijiji,Kuwashinikiza Viongozi wa Kijiji Kushiriki Maandamano Yaliotarajiwa Kufanyika Jana Hadi Ofisi za Diwani Ili Kulalamikia Mambo Mbalimbali Yanayoonekana Kuwa Kero Kwa Wananchi Hao
Hata Hivyo Maandamano Hayo Hayakuweza Kufanyika Kutokana na Viongozi wa Kijiji Kutoonekana Eneo la Tukio Hadi Kufikia Majira ya Saa Mbili na Kisha Taarifa Zikaelezwa Kuwa Viongozi Walipata Dharura ya Kuelekea Mjini Njombe Kuhudhuria Semina.
No comments:
Post a Comment